Na. Magrethy Katengu
WAZIRI wa Madini Dkt. Doto Biteko amewataka wadau wa viwanda vya madini kununua madini ya wachimbaji wadogo kwa bei elekezi ili kuepukana na baadhi yao kulalamika na kufirisika.

Dkt. Biteko agizo hilo amelitoa jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa wachimbaji wadogo wa madini na wadau wa madini ya viwandani ambapo amesema pamoja na kuwepo kwa bei elekezi wachimbaji wadogo wamekuwa wakilalamika wadau wa viwanda vya madini kununua madini yao bei ya chini
“Wenyeviwanda niwatake acheni tabia ya kuwalalia wachimbaji wadogo wadogo mnatakiwa kununua madini ya kwa bei elekezi. kwani wachimbaji wamekuwa wakilalamika kupunjwa bei”amesema Waziri
Waziri Biteko amesema kwamba makubaliano ya pamoja ya kuwa na bei elekezi ni ili mwenye kiwanda ajue bei ya kununua madini na mchimbaji ajue bei ya hivyo wenye viwanda ziingatien bei iliyowekwa o lengo likiwa ni kuwakomboa wachimbaji wadogo katika umasikini.

Akizungumzia kuhusu mkutano huo ameeleza matumaini yake ni kwamba utasaidia katika kuongeza tija kwenye usimamizi wa sekta hiyo na kuchochea kwenye ukuaji wa pato la taifa.
Ametimia fursa hiyo kuwataka wachimbaji wadogo kuharakisha madini yao yanakuwa na ubora, kwamba wapo ambao wamekuwa wakichanganya madini yao na vitu vingine ili kuongeza uzito jambo ambalo limekuwa likiwaathiri wenye viwanda.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dkt. Venance Mwasse amesema kwamba mkutano huo umekutanisha wadau watatu ambao ni wachimbaji wadogo wa madini, wenye viwanda vya madini na taasisi za kifendha.

Katika hatua nyingine STAMICO imetumia mkutano huo kuzindua mpango mkakati wa utoaji wa elimu kwa wachimbaji wadogo wa madini lengo likiwa ni kuwafikia wachimbaji wote nchini.
Kadhalika STAMICO imesaini makubaliano na makampuni yanayouza vifaa vya uchimbaji wa madini ili kuwawezesha wachimbaji hao wawe wanakodishwa vifaa hivyo kwa gharama nafuu.
Aidha Dkt. Mwasse amesema watasaini mkataba na taasisi za kifedha ili ziweze kuwakopesha mitaji wachimbaji wadogo wa madini.








