Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Taifa na mjumbe wa kamati kuu(MCC) Ndugu. Mohammed Kawaida amefunga mafunzo ya ujasiliamali yaliokuwa yanasimamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Salha Burian kupitia kikundi cha MZINGA WA MAMA SAMIA ikiwa ni moja ya shughuli katika kuadhimisha miaka 2 ya Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.
Mafunzo hayo ambayo yalikusanya vijana kutoka sehemu mbalimbali yamehitimishwa leo chini ya taasisi ya Mzinga wa Mama Samia Mkoa wa Tabora, ambayo pia yalihudhuriwa na kamati ya Usalama ya mkoa na za wilaya.
Akihutubia mamia ya vijana waliojitokeza Ndugu. Mohammed Kawaida amemshukuru na kumpongeza Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha miradi mbalimbali yenye kuwainua Vijana kwenye shughuli ya ujasiliamali.
Na kwamba serikali ya awamu ya sita, inawathamini vijana na imeweka mikakati thabiti kwa kuhakikisha miradi iliyopo inawagusa vijana. Amewataka vijana kuchangamkia fursa za mikopo ya asiliamia 10 kutoka kwenye halmashauri zetu, ili kuitumia mikopo hiyo kwenye shughuli za Ujasiliamali.
Ameuomba uongozi wa Mkoa wa Tabora kuwapa vipaumbele vijana wa mkoa wa Tabora kwenye fursa mbalimbali ili vijana hao kuwa sehemu ya miradi hiyo ili kuimarisha ulinzi wa miradi yetu. Aidha Mhe
Mkiti wa UVCCM Taifa alisimikwa Uchifu na kupewa jina la Mtemi Isike Mwanakiyungi.









