Na Magreth Mbinga
Wananchi wa Mtaa wa Ali Hassan Mwinyi wametakiwa kutoa ushirikiano kwa viongozi wao wa Mtaa na Kata na kufika ofisini endapo watapata changamoto ili ziweze kupata msaada kwa viongozi .

Hayo amezungumzwa na Diwani wa Kata ya Mikocheni Eng Nzenzely Hussein katika kikao cha kusikiliza maoni ya wananchi wa Mtaa huo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kusikiliza maoni ya wananchi wa Kata hiyo.
“Kuhusu swala la taa za barabarani tutaiandikia TARURA barua ili waweze kuweka taa na swala la matuta tayali barua imeshafikishwa tunasubiri utekelezaji hata kuhusu swala la kivuko ujenzi bado unaendelea ujenzi ukikamilika kitasaidia kuunganisha Watu wa upande mmoja na wa pili “amesema Eng Nzenzely

Pia Mtendaji wa Kata ya Mikocheni Mhe. Arodi Mmali amewataka wananchi ambao wamepata changamoto ya mkopo wa halmashauri ambao wamekidhi vigezo na bado hawajapata mpaka sasa wafike ofisi ya kata wakiwa na nyaraka zao zilizokamilika ili wapitie mfumo waone kama kuna tatizo wapatiwe msaada .
“Kuhusu swala la mapato na matumizi ni lazima kila kikao wananchi wasomewe mapato na matumizi ya mtaa wao ili waweze kufahamu fedha zao zinatumika vipi na wananchi pia muchangie ili kufanikisha shughuli za maendeleo ya Mtaa”amesema Mhe. Mmali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Ali Hassan Mwinyi Mh Benard Rwehabula amesema uongozi wa Mtaa umepokea maoni ya wananchi na utayafanyia kazi .









