Home Kitaifa KUELEKEA TUZO ZA RAIS KWA WALIPAKODI, TRA KARIAKOO YAWAPONGEZA WALIPAKODI

KUELEKEA TUZO ZA RAIS KWA WALIPAKODI, TRA KARIAKOO YAWAPONGEZA WALIPAKODI

Kariakoo, 25 Juni, 2026

Kuelekea maadhimisho ya Tuzo za Rais kwa Walipakodi Bora, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kariakoo imewapongeza walipakodi kwa mchango wao mkubwa katika ulipaji wa kodi na uzingatiaji wa sheria za kodi, hali iliyowezesha baadhi yao kutambuliwa kama walipakodi bora wa mwaka.

Akizungumza alipotembelea walipakodi meneja wa uzingatiaji wa sheria na ufuatiliaji Bw. Lihami Haule aliwashukuru walipakodi kwa kuendelea kutimiza wajibu wao kwa uaminifu na kuwataka kuendeleza utamaduni huo ili kuchangia maendeleo ya taifa na kukuza uchumi.

Nae, Meneja wa kituo cha TRA Gerezani Bi. Mercy Sijaona aliwakaribisha walipakodi kushiriki katika mbio za burudani (Fun Run) zitakazofanyika Gymkhana tarehe 27 Juni 2026 saa 12: 00 asubuhi.

Kwa upande wao, walipakodi walieleza kufurahishwa na huduma zinazotolewa na TRA, hususani utoaji wa elimu ya kodi na mwitikio wa maafisa wa mamlaka katika kutatua changamoto mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!