Home Kitaifa WAZIRI NDALICHAKO AELEKEZA UKAGUZI MAALUM, UKARABATI WA CHUO CHA WATU WENYE ULEMAVU...

WAZIRI NDALICHAKO AELEKEZA UKAGUZI MAALUM, UKARABATI WA CHUO CHA WATU WENYE ULEMAVU YOMBO.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Prof. Joyce Ndalichako ameelekeza kufanyika kwa Ukaguzi Maalum juu ya matumizi ya kiasi cha fedha shilingi milioni 694.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Prof. Joyce Ndalichako akikagua baadhi ya vifaa vya ujenzi wakati wa Ukaguzi wa ukarabati wa chuo cha Marekebisho na Ufundi Stadi kwa watu Wenye Ulemavu Cha Yombo.

Fedha zimetumika kwa ajili ya Mradi wa ukarabati wa chuo cha Marekebisho na Ufundi Stadi Yombo kwa Watu Wenye Ulemavu, jijini Dar es salaam kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19.

Mhe. Waziri Ndalichako ametoa maelekezo hayo Leo tarehe 1 Agosti, 2022 baada ya kufanya Ukaguzi wa ukarabati wa chuo hicho na kuonesha kutoridhishwa na gharama zilizotumika kununua vifaa pamoja na ubora wa vifaa vilivyotumika katika ukarabati huo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika Ukaguzi wa ukarabati wa chuo cha Marekebisho na Ufundi Stadi kwa watu Wenye Ulemavu Cha Yombo, Jijini Dar es salaam , wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ngw’ilabuzu Ludigija na Mkuu wa chuo hicho, Bi. Mariam Chellangwa
 

Mhe. Ndalichako amesisitiza yapo mapungufu makubwa ambayo ameyabaini ikiwemo kutozingatiwa kwa makadirio ya Ujenzi (BOQ), hali iliyosababisha kiasi cha fedha zilizotengwa kuisha ikiwa bado ukarabati wa ujenzi wa chuo hicho haujakamilika.

Mhe. Ndalichako amefafanua kuwa ukokotoaji wa gharama hauna uhalisia kwa mujibu wa taratibu za kutumia “Force account”.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Prof. Joyce Ndalichako akisisitiza jambo wakati wa Ukaguzi wa ukarabati wa chuo cha Marekebisho na Ufundi Stadi kwa watu Wenye Ulemavu Cha Yombo, Jijini Dar es salaam , wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ngw’ilabuzu Ludigija na Mkuu wa chuo hicho, Bi. Mariam Chellangwa
 

” Kila item inayonunuliwa imewekewa labour charge 30/%, na Contingency ya 15%, na 10% ya supervison, Sasa kwa ununuzi wa extension cable, labor charge na supervision ya nini?”

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Ngw’ilabuzu Ndatwa Ludigija, amesisitiza kuwa ataendelea kufuatilia mradi huo ili gharama zake ziendane na thamani ya fedha zilizotengwa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Prof. Joyce Ndalichako akikagua baadhi ya vifaa vya ujenzi wakati wa Ukaguzi wa ukarabati wa chuo cha Marekebisho na Ufundi Stadi kwa watu Wenye Ulemavu Cha Yombo.

Fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19, katika chuo hicho zinahusika katika ujenzi wa; Majengo ya Mabweni 2, Jengo la Darasa la Kilimo, Majengo 2 ya Nyumba za Watumishi, Jengo la Zahanati, Kituo Cha Kutwa kulelea Watoto na Karakana ya Umeme.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!