Home Kitaifa WAZALISHAJI WA POMBE KALI WANAOGHUSHI STIKA ZA TRA KUSAKWA

WAZALISHAJI WA POMBE KALI WANAOGHUSHI STIKA ZA TRA KUSAKWA

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Mwenda amesema Mamlaka hiyo itawasaka wazalishaji wa Pombe Kali maarufu kama vinywaji changamshi Bandia ambao wanaghushi Stika za TRA.

Akiwa mkoani Manyara kwa lengo la Kuwashukuru na kuwasikiliza Walipakodi, Kamishna Mkuu Mwenda amesema kughushi Stika za TRA ni makosa kisheria hivyo watawasaka wote wanaoghushi ili wachukuliwe hatua za kisheria maana uzalishaji huo unaenda sambamba na ukwepaji wa kodi.

Kamishna Mkuu Mwenda akiwa katika mkutano na wafanyabiasha mkoani Manyara amesema licha ya kukwepa kulipa kodi wazalishaji hao wa Pombe Bandia wanahatarisha usalama wa afya za watanzania kutokana na vinywaji vyao kutokuwa na viwango.

Kabla ya mkutano huo na wafanyabiasha CG Mwenda alitembelea kiwanda cha MAT cha mkoani Manyara kinachozalisha Pombe Kali maarufu kama Vinywaji changamshi na kumpongeza mmiliki wa kiwanda hicho Bw. David Mulokozi kwa kuwa Mlipakodi mzuri anayezingatia sheria.

Amesema wazalishaji wasiokuwa waaminifu wanaokiuka sheria za Nchi wamekuwa wakiwanyonya wenzao kwa kushusha bei na kuwafanya washindwe kushindana sokoni.

Kwa upande wake mmiliki wa kiwanda hicho cha MAT kinachozalisha Pombe Kali maarufu kama vinywaji changamshi Bw. David Mulokozi amesema wataendeleza ubora na kusimamia sheria za TRA katika ulipaji wa kodi.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!