Home Kitaifa WANAWAKE MARA WAPONGEZA KAZI ZA MBUNGE GHATI CHOMETE UTEKELEZAJI WA ILANI

WANAWAKE MARA WAPONGEZA KAZI ZA MBUNGE GHATI CHOMETE UTEKELEZAJI WA ILANI

Na Shomari Binda-Musoma

WANAWAKE mkoani Mara wamepongeza kazi zinazofanywa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara Ghati Chomete kwa kugusa makundi ya kijamii.

Kauli hizo wamezitoa mara baada ya kumalizika kwa kikao cha baraza la Umoja wa Wanawake( UWT) mkoa wa Mara kilichofanyika julai 7 kwenye ukumbi wa CCM mkoa.

Wanawake hao ambao pia ni wajumbe wa baraza hilo waliopokea taarifa yake ya uyekelezaji wa ilani kwa kipindi cha miezi 6 januari hadi juni mwska huu wamesema kazi anazofanya mbunge huyo zinapaswa kuigwa.

Wamesema vikindi vya wanawake vya kiuchumi amevifikia na kuwezesha shughuli zao kama ambavyo ilani ya uchaguzi ya CCM inaelekeza.

Mkumbe wa baraza hilo la UWT mkoa wa Mara na mbaraza taifa Robbi Samwelly amesema kazi zilizofanywa na mbunge Ghati zinaonekana hasa kuwafikia wanawake na jamii kwa ujumla.

Amesema yapo mambo ya kujifunza kutokana na kazi anazo zifanya za kuifikia jamii ili chama cha mapinduzi kiendelee kuaminiwa na viongozi wake.

” Mbunge Ghati amewasilisha taarifa yake kwenye baraza na imepitishwa tunampongeza kwa kazi nzuri anayoifanya”,amesema.

Mwajuma Magoti ambaye ni mjumbe pia wa baraza hilo amesema mbunge anapotimiza wajibu wake anakitengezea mazingira mazuri chama kwenye chaguzi mbalimbali.

Akiwasilisha taarifa yake kwenye baraza la UWT mkoa wa Mara mbunge Ghati Chomete moja ya mambo aliyowasilisha ni pamoja na kuendelea kuwahudumia wanawake wa mkoa wa Mara ikiwemo shughuli zao za kiuchumi.

Amesema Dkt.Rais Samia Suluhu Hassan amekudia kuwainua wananchi kiuchumi na yeye kama mbunge lazima aunge mkono juhudi zake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!