Home Kitaifa JIJI LA MWANZA LIMEADHIMISHA SIKU YA WATUMISHI

JIJI LA MWANZA LIMEADHIMISHA SIKU YA WATUMISHI

JIJI la Mwanza limeadhimisha siku ya Watumishi wa Umma kwa michezo ya aina mbalimbali huku hamasa juu ya Matumizi ya mifumo ya Tehama ikisisitizwa kupewa kipaumbele katika Utendaji wa kazi za Kila siku.

Ofisa Utumishi wa Umma Jijini Mwanza Ellah Nathan alisema leo kwenye kilele cha sherehe za Utumishi wa Umma kuwa Matumizi bora ya Tehama inatija katika Utendaji kazi za Kila siku na hivyo itawezesha Taifa kufanya Mapinduzi makubwa ya kuliletea Taifa Maendeleo.

Aliongeza kusema kuwa wametumia siku hizo kusikiliza na kutatua kero mbalimbali kwa Watumishi wao Ili kuwawezesha kuwa na Moyo wa Utendaji kazi zao za Kila siku.

Naye Kaimu Ofisa Utamaduni na Michezo katika Jiji la Mwanza Agnes Majinge alisema Watumishi wameshiriki katika michezo ya aina mbalimbali kama vile mpira wa miguu na Mikono, kuvuta kamba, ngoma, karata, bao nk.

Alisema michezo inajenga miili, inaimarisha Mahusiano na upendo miongoni mwa jamii hivyo Imekuwa faraja Kwa kada hiyo ya Utumishi wa Umma kufahamiana hivyo kuwa wamoja ambao watashirikiana katika kazi zao kwenye Halmashauri hiyo ya Jiji.

Naye Ofisa Tehama katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza Peter Juma alisema wametumia fursa hiyo vilevile kukumbushana na namna Matumizi ya teknolojia yalivyo na manufaa ya Kila siku katika kurahisisha Utendaji kazi zao.

Alitaja baadhi ya mifumo ambayo Ina manufaa ya Kila siku katika Utendaji kazi kuwa ni Tausi,Gothomis,Pepmis-Ess,Sis/Asc/Bemis/Prem,Ffars, eMrejesho na Afyass.

Juma alisema mifumo ya Tehama Imekuwa ikisisitizwa na Serikali Kila siku kutumiwa kwani kurajisisha Utendaji wa kazi za kila siku kwenye Idara za Serikali Ili kuwezesha kufikiwa Kwa Maendeleo makubwa hapa Nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!