Home Kitaifa WANAFUNZI WATAKIWA KUFICHUA VITENDO VYA UKATILI

WANAFUNZI WATAKIWA KUFICHUA VITENDO VYA UKATILI

Na Hadija Dachi

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Makambi iliyopo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wametakiwa kufichua vitendo vya ukatili na udhalilishaji watakavyobaini kutokea shuleni na katika jamii zao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyopostiwa katika ukurasa wa Instagram wa Polisi, Mkaguzi wa Polisi Kata ya Ndarima, INSP Deodat Yuda, leo Machi 10, 2026 alifika shuleni hapo akiambatana na INSP Kolandini Muhundi wa Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Songea kwa lengo la kutoa elimu kuhusu vitendo vya ukatili, unyanyasaji wa kijinsia na madhara ya uhalifu.

Amesema wanafunzi wanatakiwa kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kwa kutofumbia macho vitendo vya ukatili vinavyoweza kutokea katika mazingira ya shule na nyumbani.

Aidha, amewataka wanafunzi kutoa taarifa kwa uongozi wa shule, Dawati la Jinsia au kituo cha polisi kilicho karibu ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Pia amewahimiza wanafunzi hao kuwa wazalendo kwa kulindana wao kwa wao sambamba na kuendelea kuelimishana, hususan kuepuka vitendo vya kikatili ili waweze kutimiza malengo katika masomo na maisha kwa ujumla.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!