Na Boniface Gideon, TANGA
Wanafunzi zaidi ya 27000 kutoka Mikoa ya Tanga na Dar eS salaam wamepata fursa ya kupata Mafunzo maalumu juu ya Madhara ya ulevi hususani wa pombe huku tatizo Hilo la Unywaji pombe Nchini kwa Wanafunzi likitajwa kuw ni kubwa na chanzo kikuu kikiwa ni mfumo mbovu wa Malezi wa Wazazi.

Kupitia kampeni ya Smashed Tanzania inayolenga kutokomeza Matumizi ya Pombe kwa Wanafunzi na Kuwajengea Uwezo wa kutambua Makundi hatarishi na madhara ya Matumizi ya Pombe chini ya usimamizi wa Taasisi ya Bridge for Change Inayojihusisha na Utaoji wa Elimu ya Madhara ya ulevi wa pombe kwa Wanafunzi kwakushirikiana na Kampuni ya Vinywaji ya Serengeti Broweries Ltd pamoja na Halmashauri za maeneo husika .
Akitoa Elimu mwishoni mwa Wiki kwa Wanafunzi wa Shule za Sekondari Tanga Jiji katika Shule ya Sekondari Toledo , Mkurugenzi wa Taasisi ya Bridge for Change Ocheck Msuva Alisema tatizo la Wanafunzi Matumizi ya pombe kwa Wanafunzi sio kubwa sana kwenye Jamii ukilinganisha na Watu wazima lakini Jamii imeanza kujisahau kwakuruhusu Vishawishi vingi kwa Watoto ikiwamo kuwatuma Watoto wakanunue Pombe kuwataka Waonje na wao kama Taasisi waliliona Hilo na kuamua kuanza kutoa Elimu.

“Tunalenga kuhakikisha Mtoto anaelewa athari za Matumizi ya Pombe pia tunamuelimisha Mtoto afahamu makundi hatarishi yanayoweza kumuingiza Kwenye Matumizi ya Pombe na namna ya kuyaepuka, Elimu hii pia tunaitoa kwa Walimu ili Kuwajengea Uwezo namna Wanavyoweza kuwasaidia Watoto wasijiingize kwenye Matumizi ya Pombe” Alisema Msuva
Alisema Sehemu zote walizokwenda kutoa Elimu hiyo wamebaini uwepo wa athari za Matumizi ya Pombe huku Wanafunzi wakieleza kwa hisia Kali namna walivyoathirika kupitia Matumizi ya Pombe,
“Tumeona namna ya Wanafunzi wanavyoelezea kwa hisia Kali na vilio juu athari za Matumizi ya Pombe hii inakupa picha tu kuwa kwenye Jamii yetu Watoto wetu wanaathirika kupitia Matumizi ya Pombe utotoni, pia Halmashauri wenyewe wametuchagulia Shule ambazo wao wameona kwa namna moja ama nyengine Kuna Mazingira hatarishi zaidi ya Matumizi ya Pombe ” Alisema Msuva
Aliitaka Jamii kuhakikisha inakuwa ngao ya kumlinda Mtoto ikiwamo kumkinga na Viashiria hatarishi vinavyoweza kumfanya Mtoto kuingia kwenye Matumizi ya Pombe,
“Kila mmoja wetu ni lazima awe mlinzi kwa Mtoto kuhakikisha hawezi kujiingiza kwenye Matumizi ya Pombe, wapo Watu wanatabia ya kuwatuma Watoto wakanunue Pombe hususani Pombe za kienyeji alafu anamwambia onja kidogo Hilo ni kosa kubwa lakini pia kumtuma Mtoto akuletee pombe ni kosa , Mtoto hatakiwi kujihusisha na kitu chochote ambacho ni hatarishi kwake ikiwamo kutumwa aidha kununua au kuleta hii inamjengea ukaribu wa kushawishika kuanza Matumizi ya Pombe”Alisema Msuva
Kwaupande wake kaimu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Toledo Mjenga Kileo Alisema tatizo la Wanafunzi kujihusisha na Matumizi ya Pombe lipo japo sio kwakiwango kikubwa na kuwaomba Wadau kuendelea kutoa Elimu zaidi juu kwa Wanafunzi,
“Matumizi ya Pombe kwa Wanafunzi yapo kwenye Shule yangu , japo sio kwakiwango kikubwa Sana lakini athari zipo na tunashukuru Sana kwa kampeni hii ya kutokomeza Matumizi ya Pombe kwenye Shule zetu , Niwaombe Wadau waje kutoa Elimu zaidi pia hata Hawa Bridge for Change ikiwezekana watoe Elimu hii hata Mara 6 kwa mwaka ili kutokomeza kabisa Matumizi ya Pombe kwa Wanafunzi” Alisema Kileo
Mwisho









