Home Kitaifa “WALIOHUSIKA NA SHAMBULIO LA WAFANYAKAZI WA TRA HAWATAACHWA” – RC CHALAMILA

“WALIOHUSIKA NA SHAMBULIO LA WAFANYAKAZI WA TRA HAWATAACHWA” – RC CHALAMILA

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila amesema wahusika wote walioshiriki katika shambulio la wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kusababisha kifo cha mmoja wao hawatabaki salama.

Akizungumza wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu Amani Simbayao ambaye ni mfanyakazi wa TRA Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila amesema hasara waliyoisababisha waliofanya tukio hilo baya haina mbadala maana hakuna mbadala wa maisha ya mtu.

Mkuu wa mkoa Chalamila amesema wafanyakazi wa TRA walioshambuliwa walijitambulisha kwa mtuhumiwa na kuonyesha vitambulisho vyao lakini mtuhumiwa huyo aliamua kuwafungia vioo vya gari na kufanya mawasiliano na wenzake kabla hajachukua hatua ya kupiga kelele kwamba anatekwa ili maofisa wa TRA washambuliwe.

Ifike wakati Dola iheshimiwe, ifike wakati Dola iwe na mipaka, Amani amefungua ukurasa mpya kwenye utawala wangu kama Mkuu wa mkoa wa DSM na lazima huo ukurasa ujibu na ulete mashahidi, Mimi pamoja na Wakuu wa Wilaya kwa kushirikiana na TRA lazima mwili wa Amani utaongea, lazima Damu iliyomwagika itanena na lazima eneo palipofanyika tukio patasafishwa” Amesema Mkuu wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila akiwa msibani kwa Amani.

Watumishi wote wa TRA Tanzania watoe Sh. 10,000 kila mmoja na kununua Bondi za BOT na fedha hizo wakawa wanapita watoto kwa mujibu wa sheria kwa miaka mingi, aidha Kamishna upo au haupo na hili lipo ndani ya uwezo wenu, hili litajenga familia kujiamini na tutawasaidia watoto kuiona kesho yao kwa urahisi sana” amesema Chalamila akiwa msibani kwa Amani.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!