

Na Magrethy Katengu..
Wadau wa usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji wa wameagizwa kuhakikisha wanashirikiana na wajumbe wa Jukwaa la maji ili kusaidia kutatua changamoto zilizopo na kuandaa mipango itakayotelelezwa kwa wakati kuondo adha ya uhaba wa maji nchini.
Agizo hilo limetolewa leo Jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Jukwaa la Kitaifa la Usimamizi na Uendeshaji Raslimali Maji Mhandisi Mbogo Futakamba Wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa wadau wa maji ambao wa wamekutana kufanya Uchaguzi wa kutengeneza vikundi kazi vya watalaam vitakavyotoa ripoti ya utendaji wake kazi mwishoni mwa mwaka
“Wakati tukiendelea kukumbana na upungufu wa maji tumebaini kuwa suala la usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji bado ni changamoto kubwa hivyo kupitia jukwaa hili la Kitaifa la maji vikundi kazi vitakavyochaguliwa vitakwenda kufanya kazi na kuleta suluhisho la changamoto ya uhaba wa maji hasa kipindi cha ukame”amesema Futakamba
Hata hivyo Mhandisi Futakamba amesa kufuatia hilo wadau wa maji kupitia Jukwaa la Kitaifa la Maji linalohusisha sekta mbalimbali amesisitiza watakaochaguliwa wahakikishe wanakwenda kufanya kazi Kwa bidii hasa kazi kya kuweka mikakati ya kutafuta fedha na usimamizi madhubuti wa rasilimali hizo.

Amesema hiyo ndiyo sababu ya kuanzishwa jukwaa hilo lililokuja na programu ya kushirikisha wadau wa sekta mbalimbali kuwa sehemu ya usimamizi na uendelezaji wa raslimali hizo
“Usimamizi wa rasilimali za maji hauko vizuri, yaani hadi sasa bado tunahubiri kuhusu kutunza vyanzo vya maji, mtu anafahamu kwamba kuingiza mifugo kwenye chanzo haitakiwi, kulima jirani na chanzo cha maji ni tatizo, lakini bado wanafanya hivyo kupitia vikosi kazi vitakavyochaguliwa lazima vikasaidie wananchi juu ya umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji”amesema Mhandisi
Sambamba na hayo amesema kazi ya kusimamia Raslimali maji haipaswi kuwa ya Serikali pekee ndiyo maana jukwaa hili likaundwa kuunganisha nguvu za wadau katika kuhakikisha rasilimali hizi zinasimamiwa na kuendelezwa vizuri ipasavyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji George Lugomela amesema jukwaa hilo lina wigo mpana kwa kuongeza kuongeza ushiriki wa wadau mbalimbali ikiwemo sekta binafsi katika usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji nchini
“Jukwaa hili limewekwa kisheria na maoni yanayotolewa hapa yanapelekwa kwenye bodi ya taifa ya maji hivyo ni sehemu ambayo wadau wa sekta zote wanaweza kutoa mawazo, utaalam na ujuzi wao katika kuhakikisha maji yanaendelea kupatikana nchini “amesema Lugomela

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji George Lugomela amesema jukwaa hilo linalenga kuongeza ushiriki wa wadau ikiwemo sekta binafsi katika usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji nchini.
Naye Mratibu wa Mradi wa Global Water Leadership Asha Msoka amesema mradi huo umedhamiria kuleta Mabadiliko katika sekta ya maji kwa kujengea uwezo viongozi kupitia wadau mbalimbali na natekekeza malengo yake katika nchi kumi zilizo katika uchumi wa chini kati na Tanzania ni miongoni mwa nchi hizo
“Tunawajengea uwezo viongozi wa vikundi mbalimbali ili waweze kuchakata na kujua tatizo ama changamoto zinazozuia kufikia mengo ya kimkakati kufikia mwaka 2030 hivyo leo tunazindia vikundi vitatu vitakavyokwenda kuangalia tatizo la Uwekezaji mdogo kwenye Raslimali maji,jitihada ndogo kwenye utunzaji na usimamizi na Raslimali maji,usimamizi na Utawala kwa utunzaji maji”amesema Asha








