Home Michezo VIWANJA VITANO KUTOTUMIKA MECHI ZA LIGI KUU (NBC PREMIER LEAGUE)

VIWANJA VITANO KUTOTUMIKA MECHI ZA LIGI KUU (NBC PREMIER LEAGUE)

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesimamisha viwanja vitano kutumika kwenye mechi za Ligi Kuu ya NBC kwa kutokidhi vigezo wakati vingine vitatu vitaruhusiwa baada ya marekebisho yanayoendelea kukamilika na kupitishwa na Kamati ya Leseni za Klabu.

Viwanja vilivyosimamishwa ni Mkwawani (Tanga), Nyankumbu Girls (Geita), Ushirika (Moshi), Mabatini (Pwani), na Jamhuri (Dodoma).

Viwanja ambavyo viko kwenye marekebisho ni Majaliwa (Ruangwa, Lindi), Sokoine (Mbeya), na Kaitaba (Bukoba).

Jumla ya viwanja tisa vimepitishwa kutumika kwenye Ligi. Viwanja hivyo ni Benjamin Mkapa (Dar es Salaam), Kirumba (Mwanza), Chamazi (Dar es Salaam), Highland Estate (Mbarali, Mbeya), Karatu (Arusha), Liti (Singida), Manungu (Turiani, Morogoro), Sheikh Kaluta Amri Abeid (Arusha), na Uhuru (Dar es Salaam).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!