

Mkuu wa wilaya ya Mbulu Mhe. Kheri James amewataka wahandisi na Idara ya ujenzi kwa ujumla kuongeza umakini katika usimamizi wa miradi,ili kuhakikisha thamani ya fedha na ubora wa miradi vinazingatiwa,ili kukamilisha miradi kwa wakati,na kutoa huduma kwa ufanisi unatarajiwa na Wananchi.

Ameyasema hayo katika Ziara yake ya Ukaguzi wa Miradi katika Halimashauri ya Mji wa Mbulu, ikiwa ni Sehemu ya Maandalizi ya Mapokezi ya Mbio za Mwenge Wilayani Mbulu.
Aidha Mhe. Kheri amewasihi Viongozi wa kila Ngazi Kutenga Muda wa Kujua, na Kufatilia Miradi inayotekelezwa katika Maeneo yao na Kutoa Taarifa kwa Wananchi, na Mamlaka zinazo husika endapo watabaini Dosari ili hatua zichukuliwe kwa wakati.

Aidga Ukaguzi wa Miradi katika Halimashauri hiyo imehusisha miradi nane ya Afya, Elimu, Kilimo, Maji, Uhifadhi wa vyanzo vya maji, na Miundombinu. Ziara hii imehusisha Wajumbe wa Kamati ya Usalama, Mkurugenzi wa Halimashauri hiyo na Wataalamu.
Mwenge wa Uhuru Unatarajiwa Kupokelewa katika Halimashauri hiyo Tarehe 12 October 2023.










