
Na Deborah Lemmubi-Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Bwana Gilead Teri ameeleza kuwa Taasisi hiyo imesajili miradi 2,020 ikiwa ni ongezeko la asilimia 91,katika kipindi cha Januari 2021 hadi Januari 2025 ikilinganishwa na miradi 1,057 iliyosajiliwa kwa mwaka 2017 hadi 2020 ambayo thamani ya miradi hii inakadiliwa kuwa Dola za Kimarekani Bilioni 23.67 ikiongezeka kwa asilimia 188.7 kutoka Dola za kimarekani Bilioni 8.2 katika kipindi cha 2017-2020.
Bwana Teri ameyasema hayo leo hii Jijini Dodoma Februari 27,2025 wakati akizungumza na Wanahabari akielezea mambo 10 muhimu na ya msingi yaliyotokea katika kipindi cha Uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassan kuelekea Maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita.
Na kusema kuwa kumekuwa na ongezeko la asilimia 284.5 kutoka ajira 136,232 zilizozalishwa kipindi cha miaka minne ya kuanzia mwaka 2017 mpaka 2020, mpaka ajira 523,891 zinazotarajiwa kuzalishwa katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita kuanzia 2021-2024.
Na kuongeza kuwa kumekuwa na ongezeko la usajili wa miradi kutoka nje linalotokana na juhudi za Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuitangaza nchi na kuhamsisha uwekezaji kupitia Sera maalum ya mashirikano kupitia Diplomasia ya kiuchumi.
“Katika kipindi cha Serikali ya awamu ya Sita kati ya Januari 2021 hadi Januari 2025, TIC imesajili miradi 2,020, ambayo ni ongezeko la asilimia 91 ikilinganishwa na miradi 1,057 iliyosajiliwa katika kipindi cha 2017-2020. Thamani ya mitaji ya miradi hii inakadiriwa kuwa Dola za Marekani bilioni 23.67, ikiongezeka kwa asilimia 188.7 kutoka Dola za Marekani bilioni 8.2 katika kipindi cha 2017-2020”.
” Aidha, miradi hii inatarajiwa kutoa Ajira zilizozalishwa kutokana na usajili wa miradi kumekuwa na ongezeko la Asilimia 284.5 kutoka ajira 136,232 zilizozalishwa kipindi cha miaka minne ya kuanzia mwaka 2017 mpaka 2020 mpaka ajira 523,891 zinazotarajiwa kuzalishwa katika kipindi cha miaka minne ya awamu ya sita kuanzia 2021-2024″.
“Kumekuwa na ongezeko la usajili wa miradi kutoka nje linalotokana na juhudi zinazofanywa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuitangaza nchi na kuhamasisha uwekezaji kupitia sera yetu maalum ya mashirikano kupitia Diplomasia ya kiuchumi. Na pia ongezeko la miradi linatokana na ushiriki wa Tanzania katika makongamano mbalimbali nje ya Nchi na maboresho mbalimbali yanayofanywa na Serikali katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji Nchini.3.1 Thamani Ya MitajiThamani ya mitaji ya miradi iliyosajiliwa imepanda kwa asilimia 188.7 kutoka Dola za Marekani bilioni 8.2 hadi bilioni 23.67, ishara ya kuongezeka kwa uaminifu wa wawekezaji kwa serikali ya Awamu ya Sita”.

Aidha akiendelea kuainisha mambo ya kujivunia katika Taasisi hiyo amesema kumekuwa na ongezeko la makusanyo na mapato ambapo kwa mwaka 2022 kituo cha Uwekezaji kilikusanya wastani wa Shilingi milioni 400 kwa mwezi mmoja lakini kufika mwaka 2024 Kituo kilikusanya Bilioni 1 kwa mwezi iliyopelekea kwa mwaka 2024 kuanzia Januari hadi mwezi Desemba kukusanya zaidi ya Bilioni 12 ambao imewezesha kufungua kwa ofisi zingine za Kanda kwa Arusha na Njombe.
“Jambo lingine kubwa ambalo tumelifanya na tunajivunia ni ongezeko la makusanyo ya fedha na mapato ya Taasisi mwaka 2022 kituo cha Uwekezaji kilikuwa kinakusanya wastani wa Shilingi Milioni 400 kwa mwezi mmoja na kufikia 2024 tulikuwa tunakusanya Bilioni 1 kwa mwezi 1,kwahiyo mapato yetu kwa mwaka 2024 kuanzia Januari hadi Desemba mapato yalikuwa zaidi ya Bilioni 12 ambayo yametuwezesha kufungua Ofisi zingine za Kanda ili kuwafikia Watanzania kwa karibu,ambapo kwa mwaka jana tumefungua Ofisi Arusha na mwaka huu Februari 1 tumefungua ofisi Njombe lengo likiwa ni lile lile kufikia Watanzania kule waliko”.
Akibainisha matarajio yao kwa mwaka 2025 amesema kuwa kituo kina lengo la kusajili miradi 1500 ya uwekezaji katika kipindi cha msimu wa 2025 na kuwepo kwa malengo ya kuvutia mitaji ya kigeni yenye thamani ya Shilingi Bilioni 15.
” Matarajio ya Kituo cha Uwekezaji kwa mwaka wa 2025, yaliyowekwa katika Mpango Mkakati wake uliozinduliwa hivi karibuni ni kuwa Kwanza, kituo kina lengo la kusajili miradi elfu moja mia tano (1500) ya uwekezaji, katika kipindi cha msimu wa 2025 na kuweka malengo ya kuvutia mitaji ya kigeni yenye thamani ya bilioni 15. Pia TIC imejipanga kuhakikisha kwamba, angalau asilimia kumi ya miradi iliyosajiliwa inalenga katika kuchangia juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuonyesha jitihada za kituo hicho za kusukuma mbele uwekezaji wenye manufaa na endelevu”.
Katika mgawanyo wa Umiliki katika miradi kwa kipindi cha Januari 2021 hadi Januari 2025 amesema kuwa asilimia 34.3 inamilikiwa na Watanzania, asilimia 42.6 ni ya wageni na asilimia 23.1 ni miradi ya ubia kati ya Watanzania na wageni ambao ni tofauti na ukilinganisha iliyosajiliwa kwa kipindi cha mwaka 20217-2020.
“Mgawanyo wa Umiliki katika Miradi ya Uwekezaji kwa kipindi cha Januari 2021 hadi Januari, 2025Katika miradi hii, asilimia 34.3 inamilikiwa na Watanzania, asilimia 42.6 ni ya wageni, na asilimia 23.1 ni miradi ya ubia kati ya Watanzania na wageni ukilinganisha na miradi iliyosajiliwa katika kipindi cha kuanzia 2017 hadi 2020 ambapo asilimia 27.4 inamilikiwa na Watanzania, asilimia 44.1 ni ya wageni, na asilimia 28.5 ni miradi ya ubia kati ya Watanzania na wageni.Juhudi zilizofanywa na serikali ya awamu ya sita kushusha kiwango cha chini cha kuruhusu kusajili mradi Kituo cha Uwekezaji ili kupata vivutio kutoka dola za Marekani laki moja mpaka dola 50,000 kimesaidia kuongeza usajili wa miradi ya wawekezaji wa ndani.
Kituo cha Uwekezaji Tanzania kimeanzishwa chini ya sheria ya Uwekezaji kikiwa na majukumu ya kuratibu, kuhamasisha, na kuhudumia wawekezaji kwa kutoa huduma mbalimbali ikiwemo kutoa vibali, leseni na usajili wa uwekezaji kupitia Kituo cha Mahali Pamoja (One Stop Facilitation Centre).ambapo pia TIC na jukumu la kukusanya, kuchambua, kuhamasisha na kusambaza taarifa za fursa za uwekezaji zinazopatikana hapa nchini na vilevile ina wajibu wa kuishauri Serikali kuhusu kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini.
