BENKI ya Biashara ya Taifa TCB imesema itaendelea kuunga mkono serikali katika miradi yake ya kimkakati kwa kuhakikisha wanagusa maisha ya watanzania katika kila sekta ikiwemo sekta ya kilimo, ambapo mpaka kufikia June 2024 benki hiyo imeweza kutoa mikopo ya jumla kiasi cha shilingi Trilioni 1.2Â lakini katika hizo kuna shilingi bilioni 44 zilizokwenda kwenye sekta ya kilimo japo inafahamika kuwa mnyororo wa kilimo ni mpana, na fedha hizo ni zile zilizoorodheshwa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika siku ya ushirika duniani mkoani Tabora Meneja Mkuu wa TCB Bw. Korimba Tawa ameeleza kuwa Benki hiyo mbali na fedha hizo zilizotegwa mnyororo wa kilimo ni mpana na kupitia vyama vya upili wana ushirika wanapata huduma mbalimbali zikiwemo huduma za kibenki zinazopelekea kukuza mnyororo huo.
“Ushindani sokoni ni mkubwa lakini TCB tumekua tukifuata na kufanya miradi ya kimkakati ya serikali kwa kuhakikisha wana ushirika na watanzania wote na miradi yote inahudumiwa, kwa benki kutoa mikopo yenye riba nafuu (Single digits) hii ni njia pekee ya kumfanya mwanaushirika achague TCB ” anasema
Katika hatua nyingine Tawa anaeleza kuwa pamoja na miradi mingine TCB imekua ni mshirika mkuu wa mradi wa maendeleo wa SGR ,lengo kuu ikiwa ni kufikia adhma ya serikali ya kuhakikisha kila Mtanzania anashirikishwa kwenye ujumuishwaji wa kifedha ili kuleta maendeleo.
” TCB inahusika katika kuwapa mitaji wanaushirika kwa maana ya kuwawezesha katika pembejeo na mnyororo mzima wa ushirika, sambamba na kuhudumia pia katika stakabadhi za ghala,na pia kuna kitengo kinachohusika na ushirika na upande wa mikopo,kwa kuwawezesha,masoko na pia kuwaongezea mtaji“anasema
Kwa upande wake meneja wa tawi la TCB Tabora Bw. Timony Joseph amesema kuwa watahakikisha kuwa wanatoa huduma kwa wana ushirika wote wenye uhitaji wa kuhudumiwa na TCB , na kuhusu stakabadhi ghalani mpaka sasa wamekwisha hudumia kiasi cha shilingi bilioni 23,na pia wamepanga kuwafikia wana ushirika mmoja mmoja kuweza kupata huduma za TCB.
“Tumekua tukitoa huduma mbalimbali katika sekta ya ushirika zikiwemo za ufunguaji wa akaunti,uwezeshaji wa mikopo,uwekaji akiba baada ya kuuza mazao. Lakini pia usaidizi wa upatikanaji wa masoko Pembejeo,,uwezeshwaji wa kukuza kilimo na mengineyo“anasema Timony
TCB ilianza kujihusisha na mambo ya ushirika tangu mwaka 1990 kupitia mradi wa kaempu uliokuwepo mkoa wa Kagera na hivi sasa TCB imekua mstari wa mbele katika kutoa pembejeo, mikopo kwa wana ushirika na wafanyakazi kupitia mikoa ya kusini, kaskazini, magharibi , Kigoma, Shinyanga lakini pia kupitia Amcos pamoja na vyama vya msingi.
Ni mchakato mzuri Kwa Taifa letu,nimefurahi hiyo huduma je Mimi kama mkulima nakipataje nko Rukwa , Ahsante