Home Kitaifa TANZANIA, SAUDI ARABIA KUIMARISHA BIASHARA NA UWEKEZAJI

TANZANIA, SAUDI ARABIA KUIMARISHA BIASHARA NA UWEKEZAJI

Serikali ya Tanzania na Ufalme wa Saudi Arabia zimekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji, kwa lengo la kufungua fursa mpya za kiuchumi na kukuza sekta ya viwanda nchini.

Makubaliano hayo yamefanyika, Machi 13, 2026,
wakati wa mazungumzo kati ya Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo na Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania Mhe. Yahya Ahmed Okeish, yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, pande zote mbili zimeazimia kuelekeza nguvu katika uanzishaji na uendelezaji wa Kongani za Viwanda vitakavyolenga kuongeza thamani ya mazao ya kilimo na mifugo, kukuza uhaulishaji wa teknolojia, pamoja na kupanua wigo wa masoko ya bidhaa za Tanzania nchini Saudi Arabia

Pamoja na hayo, viongozi hao wamekubaliana kuimarisha usafiri wa anga kwa kuwa na safari za ndege za moja kwa moja kutoka Tanzania hadi Saudi Arabia, hatua inayotajwa kuwa kichocheo na kurahisishai ufanyaji biashara na uwekezaji wawekezaji baina ya nchi hizo mbili.

Kwa upande mwingine. Londo na Balozi Okeish walijadiliana kuhusu maandalizi na ushiriki wa Tanzania katika Maonyesho ya Kimataifa ya Expo 2030, yatakayofanyika jijini Riyadh kuanzia Oktoba 2030 hadi Machi 2031.

Londo alibainisha kuwa Tanzania inachukulia maonyesho hayo kama fursa ya kimkakati na “lango” muhimu la kuionyesha dunia bidhaa, huduma, na vivutio mbalimbali vinavyopatikana nchini na hivyo kuvutia biashara na uwekezaji nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!