Home Kitaifa TANI 1100 ZA UFUTA ZIMEUZWA PWANI KATIKA MNADA WA NNE KWA SHILINGI...

TANI 1100 ZA UFUTA ZIMEUZWA PWANI KATIKA MNADA WA NNE KWA SHILINGI 3280/- KWA KILO

Tani 1100 za zao la ufuta zimeuzwa katika mnada wa nne wa msimu wa mwaka 2024/25 kwa bei ya shilingi 3280.13 kwa kilo Moja huko mkoani Pwani.

Akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari mara baada ya mnada Meneja wa Chama kikuu Cha ushirika wa Wakulima wa mkoa wa Pwani CORECU Hamisi Mantawela huko katika mnada wa nne wa ufuta mkoa wa Pwani Katika ghala la CORECU Wilaya ya Kibiti amesema wakulima wa zao hilo la ufuta wameridhia kuuza ufuta wao kwa bei ya wastani ya Sh. 3280.13, ambapo hizo Tani 1100 zimeuzwa.

Alisema maboresho ya minada ya ufuta kupitia mfumo wa TMX yanaendelea kwa kutoa mafunzo kwa Maafisa Tehama na masoko wa Vyama vya ushirika nchini.

Mantawela alisema serikali inachofanya kwasasa ni kuboresha mfumo wa TMX ilikumhakikishia mkulima anapata faida katika mauzo ya ufuta wake kwa kuuza kidigitali badala ya kuuza kwa mfumo wa kizamani wakutumia mabahasha mengi minadani.

Aidha ameeleza kuwa kuwa utekelezaji wa Mfumo huo ulitarajiwa kuanza mwezi Julai mosi mwaka huu, Kwa kutoa mafunzo Kwa watendaji, Ili minada inayokuja iweze kutumia Mfumo huo kwa ufasaha zaidi.

Akijibu malalamiko ya Wakulima wa ufuta mkoa wa Pwani Mantawela alisema serikali Kufuatia malalalamiko ya wakulima wa Ufuta mkoani Pwani kwamba baada ya kikao cha Wadau na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, kwamba Mfumo huo baada ya Mafunzo utaboreshwa.

“Baada ya Mafunzo inawezekana serikali ikaja na utekelezaji wa hayo maboresho ya mfumo kwenye vyama vikuu, na vyama vya ushirika na itajulikana kwamba ufuta utauzwa Kama Mfumo wa zaman au kwa mfumo wa kidigitali TMX” alisema Mantawela.

Kuhusu ufuta unaobaki katika minada Meneja huyo wa CORECU alisema ufuta utakao baki kwenye minada kuanzia Sasa mnada husika kwa kushirikiana na wakulima na uongozi wa Chama wataweza kumpigia simu mnunuzi wanaemtaka aliyeshiriki ununuzi kwenye mnada na kumshawishi anunue ufuta huo uliobaki.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CORECU Mussa Ng’eresa ametoa shukurani Kwa serikali Kwa kupokea changamoto za wakulima wa Ufuta Pwani na kuzitolea ufafanuzi Ili wakulima waweze kunufaika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!