Home Kitaifa CPA MAKALA JITIHADA ZA SERIKALI KUONA UBORESHWAJI WA HUDUMA NCHINI

CPA MAKALA JITIHADA ZA SERIKALI KUONA UBORESHWAJI WA HUDUMA NCHINI

Na Mariam Muhando Dar es salaam.

Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi CCM CPA Amos Makala Amesema Jitihada za serikali ni kuona uboreshaji wa huduma mbalimbali zinapatikana ili Wananchi waepukane na changamoto.

CPA Makala meyasema hayo Leo Tarehe 08 Julai 2024 katika ziara yake ya pili ya kusikiliza kero za wananchi Jimbo la Segerea liliopo Wilaya ya Ilala Jijini Dar es salaam ambapo amesema Maendeleo yanaonekana kwa jitihada za serikali ya awamu ya sita chini ya Usimamizi wa Rais Dr Samia suluhu Hassan.

“Haya ni maendeleo makubwa sana na tunaendelea kumpongeza Rais Samia Kwa kazi kubwa anayoifanya kwenye huduma tulizoziona hapa na Vipimo tulivyoviona hapa ni vya kisasa vya hali ya juu magonjwa yote,operesheni ndogondogo zinafanyika,wodi za kinamama za wazazi ni nzuri tumeona,kliniki zinavyoendelea,na Wagonjwa wanavyopata huduma”, Amesema Makala

Mwenezi ametembelea miradi mbalimbali ikiwemo Mradi wa Shule ya sekondari ya Minazi mirefu iliyojengwa kwa gorofa na Zahanati ya kisasa ya Kinyerezi ambapo ziara hiyo Bado inaendelea Kwa kuhitimishwa katika Viwanja vya Liwiti ili kusikiliza kero za Wananchi na kuzipatia Ufumbuzi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!