Home Michezo TAIFA STARS YAPOTEZA MECHI YA NNE MFULULIZO,YACHAPWA NA IRAN

TAIFA STARS YAPOTEZA MECHI YA NNE MFULULIZO,YACHAPWA NA IRAN

TIMU  ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeendelea kupata matokeo mabaya baada ya kupoteza mchezo wake wa nne mfululizo, kufuatia kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Iran katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa leo Jumanne, Oktoba 14, mjini Dubai.

Stars, ambayo haijapata ushindi tangu ilipotolewa kwenye hatua ya robo fainali ya CHAN 2024 kwa kufungwa na Morocco bao 1-0, imekuwa ikisuasua pia katika michezo ya kufuzu Kombe la Dunia, ikipoteza mechi mbili mfululizo dhidi ya Niger na Zambia kwa matokeo kama hayo.

Matokeo haya yanazidisha presha kwa Kocha Hemed Morocco, ambaye alikabidhiwa majukumu ya kuinoa timu hiyo baada ya kuondoka kwa kocha wa zamani kutoka Algeria, Adel Amrouche, mwaka 2024.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!