Home Burudani Sifa Gospel Fest Kung’ara Dar Es Salaam Desemba 4

Sifa Gospel Fest Kung’ara Dar Es Salaam Desemba 4

Celebrating 25 Years of NHIF

WAPENZI wa muziki wa Injili wanatarajiwa kukutana katika tamasha la Sifa Gospel Fest 2026, litakalofanyika Desemba 4, mwaka huu, katika Viwanja vya Posta Kijitonyama, Dar es Salaam, likiwa kilele cha ziara ya ibada ya kusifu na kuabudu iliyofanyika katika mikoa mitano nchini.

FAHARI AFYA

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Novemba 24, 2026, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Suma Mwaitenda, amesema waimbaji na watumishi wa Mungu watakaohudumu ni pamoja na Bon Mwaitege, Paul Clement, Rose Mhando, Upendo Nkone, Bella Kombo, Godfrey Steven na Boaz Danken.

Amesema tamasha hilo lenye kaulimbiu ya “Kila Mwenye Pumzi Amsifu Bwana” litashirikisha pia kwaya na bendi mbalimbali za muziki wa Injili, zikiwemo The Healing Missionaries, Agape Gospel Band, Mafunuo Kwaya na Moravian Efata.

Ameeleza kuwa ziara hiyo iliyoanza Mbeya Septemba mwaka huu imepita katika mikoa ya Geita, Mwanza, Arusha na Dodoma, huku Dar es Salaam ikiwa mkoa wa sita na wa mwisho katika ziara hiyo.

Tofauti na matamasha mengine yanayochanganya mahubiri na uimbaji, Sifa Gospel Fest itajikita katika nyimbo za sifa na kuabudu, kwa lengo la kuwaunganisha waimbaji na watumishi wa Mungu katika jukwaa moja.

Aidha, amesema kutakuwa na shughuli tatu kuu ambazo ni kongamano la vijana kuhusu ujasiriamali, michezo na burudani kwa watoto na vijana, pamoja na kilele cha tamasha hilo kitakachofanyika kupitia Usiku wa Sifa.

Amesema tamasha hilo halitakuwa na kiingilio, hivyo wananchi wote wanakaribishwa kushiriki katika tukio hilo la kumsifu na kumwabudu Mungu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!