Home Kitaifa SHILOLE ALAMBA SHAVU LA UBALOZI KAMPUNI YA MIKA MEATS

SHILOLE ALAMBA SHAVU LA UBALOZI KAMPUNI YA MIKA MEATS

Na Magrethy Katengu

Zuwena Mohamodi kwa jina la Kisanii Shilole Maarufu ( Shishi Baby) amekabidhiwa kuwa balozi wa Kampuni ya Mika Meats inayojihusisha na biashara ya nyama ikiwemo ya Mbuzi, Ng’ombe, Samaki, Kondoo kuku.

Akizungumza leo Jijini Dar Dar es salaam Mstahiki Meya Omary Kumbilamoto wakati wa ufunguzi wa bucha jipya liliko Posta Jijini Dar es salaam amesema Shilole amekuwa binti pekee mfano wa kuigwa anayefanya kazi za mama lishe kupika na kuuza chakula na ameiheshisha sana kazi ambayo miaka ya nyuma waliokuwa wanaifanya walikuwa wakidharaulika hivyo sasa inaheshimika hadi wanaume wanaifanya ..

Mika meats ni Wauzaji wa nyama zinazozalishwa hapa hapa nchini na na wanamipango mikubwa ya baadae kuanza kufuga wenyewe huku wakiongeza wigo wa kuanzisha bucha 1000 nchi zima ambapo watauza kwa gharama nafuu kuanzi pakeji ya 2000 kilo bei yake sawa na Vingunguti machinjioni” amesema Meya

Hata hivyo wakati Mstahiki Meya amemshuru Shilole kwa kukitolea kuwaninulia Mama lishe 20 Kila mmoja kilo tano za nyama wakafanye bishara ya chakula ameguswa kwani biblia inasema Amsaidiaye Masikini amemkopesha Mungu hivyo uthubutu alioufanya kuwasaidia watu hao ni jambo la pekee.

Naye Balozi wa Mika Meats Zuena Mohamedi Jina Maarufu Shilole amesema yeye ni Mama lishe kwani anaipenda kazi yake hajawahi ijutia hivyo pia ameshukuru Kampuni Mika Meat kwa kumuona kuwa anafaa kuwa balozi wao hivyo watarajie kuona mambo makubwa kupitia yeye wateja watamiminika kununua chakula pamoja na mboga katika bucha zote 9 zilozopo Dar es salaam..

Naye Mwanasheria wa Kampuni hiyo Mika Meats Wakili Baraka Mase amesema Kampuni hiyo imesajiliwa kisheria na inajihusisha na uuzaji wa nyama na samaki Bei ni nafuu hivyo hadi shilole anakabidhiwa Ubalozi na vyombo vya habari vinashuhudia hakuna ubabaishaji na imejipanga kufuga mifugo wenyewe na kuchinja na wameajiri aslimia 90 ya watanzania.

Kwa upande wao baadhi ya mama lishe waliohudhuria hafla hiyo akiwemo Rose Maungo kutoka Tegeta Anna Kuyenge Weshukuru Kampuni hiyo kwa kuwasogezea bidhaa karibu na kuwaizia kwa bei nafuu hivyo wamewaomba wawe wanawakopesha kwani wao hawana mitaji wamezoea wanachukua bidhaa asubuhi jioni wakishamaliza kuuza chakula wanalipa walipokopa ikiwemo mchele, unga, Mafuta ya kula , na nyama hivyo waliangalie hilo kwa jicho la tatu ili wawe wateja wao .

Aidha Kampuni ya Mika Meats ina bucha 9 katika mkoa wa Dar es salaam na wanampango baada miaka mitano wawe bucha 50 mwishoni mwa mwaka huu na bucha 1000 miaka mitano ijayo hivyo na kuanza kufuga mifugo wenyewe tayari wameshanunua mashamba ya kufugia hivyo Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imefungua milango ya uwekezaji ni mwendo kwa kazi tu na kuibua fursa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!