Home Kitaifa SHAIRI LA SALAMU ZA MWAKA MPYA 2025 KUTOKA KWA MWANDISHI SHOMARI BINDA

SHAIRI LA SALAMU ZA MWAKA MPYA 2025 KUTOKA KWA MWANDISHI SHOMARI BINDA

Nianze na shukrani,kwa Mola wetu Karima
Kututia uzimani,kwa pumzi yake kuhema
Mwaka umetamatani,nasi bado tuwazima
Salamu za mwaka mpya,nawasalimu wapendwa

Nasalimu visiwani,bara siwaachi nyuma
Nawasalimu wandani,marijali wakuhema
Binda ninazisaini,zifike kwenu mapema
Salamu za mwaka mpya, nawasalimu wapendwa

Ni mapito duniani,wengine wameihama
Anatupenda Manani,pumzi haijasimama
Sisi tumlipe nini, ibada zije simama
Salamu za mwaka mpya, nawasalimu wapendwa

Changamoto mitihani,twashukuru kwa uzima
Ni mapito duniani,mwanadamu uwe mwema
Ukipata hamsini,uushukuru uzima
Salamu za mwaka mpya, nawasalimu wapendwa

Tupendane duniani,tusipeane lawama
Akikujia jirani,kwa jambo lime mkwama
Msaada ndio dini,sio kumpa kilema
Salamu za mwaka mpya, nawasalimu wapendwa

Tuombe ishilini tano,uwe mwaka wa neema
Tuzidishe mapambano,kazi iweze simama
Maisha yawe manono,tusiwe wenye kukwama
Salamu za mwaka mpya, nawasalimu wapendwa

Nimefika tamatini,uwe mwaka wa salama
Tumuombeni manani,tumalize kwa salama
Mabaya tusitamani,utu tukaja uzima
Salamu za mwaka mpya, nawasalimu wapendwa

Shairi hili limetungwa na Shomari Binda( Mvubula Vinongo)0755487117/0672687117

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!