Home Kitaifa SERIKALI YAWATAKA WENYE VIWANDA KUIJALI NA KUILINDA NGUVU KAZI.

SERIKALI YAWATAKA WENYE VIWANDA KUIJALI NA KUILINDA NGUVU KAZI.

Serikali imewataka wamiliki wa viwanda nchini kujali na kulinda nguvukazi inayotumika katika uzalishaji ili na uzalishaji endelevu wenye tija kwa maendeleo endelevu.

Tamko hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Patrobas Katambi,alipofanya ziara katika viwanda mbalimbali Jijini Dar es salaam akiwa ameambatana na Maafisa wa Taasisi chini ya ofisi ya Waziri Mkuu ikiwemo Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA)

Akizungumza katika ziara hiyo Mhe.katambi amesema malengo ya Seraikali ya awamu ya sita ni kuchochea ukuaji wa uchumi wa Nchi kupitia uzalishaji viwandani ambapo Serikali inawajibika kujenga mazingira bora ya biashara na uwekezaji.

“Sisi kama Serikali tunajitahidi kuhakikisha kwamba kunakuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji pamoja na kuhakikisha kwamba shughuli zote za uwekezaji zinazingatia sheria za nchi ikiwemo sheria za Ajira na Mahusiano kazini,usalama na afya mahali pa kazi, na hifadhi kwa jamii”amesema Naibu Waziri na kuongeza

“Katika ziara hii ya leo tumefanya ukaguzi wa kushtukiza katika viwanda vitano vinavyozalisha bidhaa mbalimbali zikiwemo bidhaa za plastiki ambapo tumebaini mapungufu mengi katika viwanda husika ikiwemo mazingira ya kazi yasiyo rafiki kwa wafanyakazi na uwepo wa vitendo vya unyanyasaji kwa watumishi, hivyo nitoe rai kwa waajiri wote nchini kuhakikisha kwamba wanatoa ajira zenye staha ili kuendana na Sheria za nchi pamoja na mikataba ya kimataifa ambayo nchi yetu imeridhia”.

Aidha Katambi amewakaribisha wawekezaji wenye changamoto mbalimbali katika shughuli zao kuziwasilisha Serikalini ili ziweze kupatiwa ufumbuzi na hivyo kuondokana na vikwazo katika uzalishaji.

Kwa upande wake Meneja wa Kanda ya Pwani OSHA,bwana George Chali ameainisha changamoto za usalama na afya zilizo bainika katika ziara hiyo zikiwemo ukosefu wa vifaa Kinga mikononi mwa wafanyakazi,uwepo wa nafasi finyu za kufanyia kazi na wafanyakazi kutekeleza majukumu yao katika mtindo usiofaa kiusalama na afya(ergonomic issues).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!