Home Kitaifa SERIKALI YAPONGEZA UWEKEZAJI WA NYIHITA SUNFLOWER UPATIKANAJI WA MAFUTA YA KULA

SERIKALI YAPONGEZA UWEKEZAJI WA NYIHITA SUNFLOWER UPATIKANAJI WA MAFUTA YA KULA

Na Shomari Binda-Rorya

SERIKALI imepongeza uwekezaji uliofanywa na muwekezaji Nyihita Wilfred wa uanzishaji wa kiwanda na mashamba kwaajili ya uzalishaji wa mafuta ya alizeti.

Pongezi hizo zimetolewa jana februari 26 na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exauds Kigahe alipotembelea mashamba na kiwanda cha Nyihita Sunflower wilayani Butiama na Rorya.

Akizungumza mara baada ya kutembelea maeneo hayo amesema Tanzania bado ina upungufu wa viwanda vya mafuta ya kula hivyo wawekezaji wakiwemo wa ndani wanapaswa kulindwa.

Amesema mkurugenzi Nyihita amefanya jitihada kubwa kwani licha ya kufanya uzalishaji lakini amekuwa msaada wa kwa kuanzisha programu za kuwasaidia wakulima kupitia kiwanda alichoanzisha.

Kigahe amesema serikali itaendelea kuunga mkono jitihada za uwekezaji unaofanyika kuhakikisha viwanda vilivyoanzishwa vinaendelea.

Amesema suala la upatikanaji wa mali ghafi kwaajili ya uzalishaji ni muhimu hivyo suala la kilimo cha umwagiliaji ni muhimu.

” Nimshukuru na kumpongeza sana Nyihita kwa uwekezaji aliofanya wa upatikaji wa mafuta ya kula kupitia zao la alizeti.

” Tena kupitia uwekezaji wake anawasaidia na wakulima kwa kueka mtambo kiwandani kwake ili nao wakamue mafuta yao kwenye sehemu ya mazao wanayo uzia kiwanda”,amesema.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kiwanda cha Nyihita Sunflower,Nyihita Wilfred amesema lengo la kuwasaidia wa kulima kwa kuwawekea mashine ya ukamuaji wa mafuta ni kuona nao wanainuka.

Amesema mkuluma zckipata motisha kutokana na kile anachokifanya inamuongezea ari ya kulima zaidi.

Nyihita amesema suala la upatikanaji wa mali ghafi ni muhimu hivyo serikali inapaswa kuendelea kufanya juhudi za kuwasaidia wakulima kwa kufanya kilimo biashara.

Katika ziara yake ya kikazi ya siku 3 mkoani Mara Naibu Waziri Kigahe ametembelea pia viwanda vya samaki na maziwa vilivyokufa mkoani Mara kwaajili ya kuona changamoto zake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!