Na Shomari Binda-Musoma
MWENYEKITI wa zamani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mara Christopher Sanya ameishukuru jumuiya ya wazazi mkoa wa Mara kumualika kwenye baraza lake.
Licha ya kushukuru kualikwa kwenye baraza hilo la mkoa ametoa ushauri namna ya kupatikana kwa viongozi kupitia mikono ya wazazi.
Amesema jumuiya ya wazazi ni sehemu ya malezi hivyo kuna umuhimu mkubwa kupata kuona aina ya viongozi wanaotakiwa kuwaongoza wananchi.
Sanya amesema jumuiya ya wazazi inapaswa kupitia na kuona fomu za wagombea wanaoomba nafasi mbalimbali.
“Naishukuru jumuiya ya wazazi mkoa wa Mara kwa kunikumbuka na kunikumbuka na mimi bado nipo sijastafu siasa na tutaendelea Kuwa pamoja”
“Jumuiya yetu imekuwa ikipanda na kushuka kutokana na aina ya viongozi wanaokuwa madarakani naamini waliopo kwa sasa mambo yatakwenda vizuri” amesema Sanya
Mwenyekuti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mara,Kambarage Magubo,amemshukuru Sanya kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa Chama na jumuiya zake.
Amesema Sanya ni kiongozi mzuri ambaye jumuiya itaendelea kumtumia katika shughuli mbalimbali kwa kuwa ni kiongozi makini.
Akifungua baraza hilo la kwanza,Mjumbe wa Baraza la Wazazi Taifa na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Taifa Edwin Peter amesema jumuiya ya wazazi mkoa wa Mara inafanya vizuri miongoni mwa jumuiya Tanzania
Amesema vikao ndio umuhimu wa baraza na kuwaomba wajumbe kushirikiana na viongozi ili kuona mambo yanasonga na jumuiya kuimalika.









