Na Theophilida Felician Kagera.
Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe Albert Chalamila aagiza kuwatafuta watoto wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za Sekondari Mkoani humo kwa mwaka wa (2023) ili waweze kuripoti kabla ya kuisha kwa mwezi huu wa January.
Akitoa maagizo hayo kwa waandishi wa habari katika maeneo ya ofisi ya mkoani Kagera Manispaa ya Bukoba Chalamila amesema kuwa jumla ya watoto waliochaguliwa kujiunga na masomo ya Sekondari kwa mwaka wa 2023 ni watoto Elfu (59175) waliokwisha ripoti mpaka sasa ni watoto (35526) sawa na (60%) pekee ( 40%) bado hawajaripoti katika shule zao ambapo wilaya ya Biharamulo ni ya mwisho katika zoezi hilo kwani watoto waliokwisharipoti ni 45% tuu kati ya watoto wote waliochaguliwa kujiunga na shule za sekondary wilayani humo.

Awali maagizo yake ameeyaelekeza kwa wakuu wa wilaya, wakurugenzi, maafisa elimu, waratibu elimu kata, tarafa, walimu wakuu na viongozi wengine wakiwemo wenye viti wa Halmashauri, madiwani sambamba na wenye viti wa vijiji na mitaa wote kushirikiana na kufanya msako wa nyumba kwa nyumba ili kuweza kuwabaini watoto wote ambao hawajaripoti ili waweze kuripoti haraka iwezekanavyo.
Pia amewaelekeza wakuu wawilaya , wakurugenzi kuhakikisha wanapokea taarifa za wanafunzi walioripoti kwa kila siku kutoka kwa wakuu wa shule husika huku akiwataka wakuu washule kutokukiuka utaratibu wakuanzisha michango kwa wazazi ambayo haiko kwenye utaratibu badala yake wawashirikishe wazazi katika suala zima la kutoa chakula cha mchana kwa watoto kwani ni hitaji muhimu sana kwao “naomba niludie chakula kwa wanafunzi si mchango bali ni hitaji la msingi kama mavazi, kama usingizi mtu anapohitaji kulala chakuka simchango chakula ni hitaji la msingi”akisisiza hayo kwa waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila.
“Mkuu wa shule yeyote atakaye wa kwaza wazazi kwakuanzisha michango ambayo haipo kwenye utaratibu na kuweka msimamo wa kutokumpokea mwanafunzi kwa sababu hana michango atatimuliwa cheo chake na kuchukuliwa hatua za kinidhamu” amesema Mkuu wa mkoa Chalamila.
Hata hivyo ameongeza kusema kuwa
wazazi na walezi watakaobainika kuwaficha watoto wao wasiende shule ili wawasaidie katika shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Mbali na hayo amefafanua kuwa Serikali chini ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassani imekuwa ikitumia nguvu nyingi ya kuwekeza kiwango kikubwa cha fedha Kagera katika kujenzi wa miundo mbinu ya madarasa (881) kwa awamu ya kwanza, wamu ya pili madara ( 514) , nyumba za walimu, vyoo, maabara hivyo hakuna sababu ya watoto kubakia majumbani bila yakwenda shule.








