Na Theophilida Felician Kagera.
Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe Albert Chalamila amekabidhi jumla ya pikipiki 342 zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni moja kwa maafisa ughani kuanzia ngazi ya Wilaya, Kata na Vijiji.
RC Chalamila amekabidhi pikipiki hizo leo Tarehe 27 January mwaka huu katika Manispaa ya Bukoba.
Mkuu huyo wa Mkoa kabla ya kuwakabidhi pikipiki ametoa maelekezo kwa wakurugenzi akitoa maagizo akisema kuwa “Ninyi wakurugenzi mmekuwa wavivu na hela yenu inawauma sana kutenga kwenye kilimo inapokuja suala zima la bajeti katika kilimo hamziwekagi kabisa afisa ughani labda akija kuomba mafuta inakuwa ni kelele nongwa aaaa! mapikipiki yenu haya nayo! niwambieni hizi ni pikipiki ambazo amezitoa Mhe Rais manake ni kwamba wekeni utaratibu mzuri wa namna gani maafisa hawa na vyombo hivi vinaweza kuwa salama lakini vikafika kwa watu ili viweze kutoa elimu iliyokusudiwa” amesema Mkuu wa Mkoa Chalamila huku wakimpigia makofi mazito maafisa hao wa kilimo.

Aidha amewaagiza tena wakurungezi hao hao ya kwamba pikipiki hizo zisitumike kabla ya kuwapatia mafunzo ya udereva maafisa kilimo jambo ambalo litawasaidia kuziendesha kwa usalama zaidi.
Jambo jingine amewaagiza kufanya vikao vya mara kwa mara na maafisa kilimo ili kuwapatia taarifa za kila mwezi juu ya huduma za utendaji kazi walizozitoa kwa wakulima hali itakayosaidia kutathimini maendeleo ya uajibikaji wao.
Amewasihi maafisa ughani kuzitumia kwa umakini pikipiki kwakuziendesha kwa mwendo wa kawaida bila kuzidisha kasi ya mwendo watakapokuwa kwenye majukumu yao ili kuepusha madhara ya ajari, hiyo ikiwa ni sambamba na kuzitunza vizuri ili ziweze kudumu zaidi.

Amewakumbusha kuwa waende wakawajibike vyema katika kuwafikia wananchi na kutoa elimu ya kilimo hali itakayosaidia kuwaondolea changamoto zao ikiwemo kushughulikia masoko ya mazao yao.
Hata hivyo ameongeza kuwa Mhe Rais ametoa pikipiki hizo kwenye sekta ya kilimo kwa malengo ya kuendelea kuchochea upatikanaji wa suala la ajira kwa vijana na makundi mengine na kupunguza malalamiko ambayo yamekuwa yakijitokeza ya ukosefu wa ajira hivyo kilimo kitawezesha watu kujikita katika sekta hiyo ambayo imepewa kipaumbele kwa sasa kupitia nyanja mbalimbali
Kwa upende wake Katibu tawala wa Mkoa Kagera Mhe Toba Nguvula amewaeleza maafisa hao juu ya kipaumbele kikubwa alichokitamka Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassani ni kupanua wigo mkubwa wa uzalishaji wa mazao kwa adhima ya kujitosheleza kwa mazao ya chakula hapa nchini na Kagera kwa ujumla.
Katibu tawala huyo amewahimiza maafisa hao kwamba pikipiki hizo zimelenga kwenda kuwafikia wakulima wote wa Mkoa huo na sikwa kitu kingine.
“Hizi pikipiki lengo lake ni kukufanya wewe Afisa ughani ufike eneo la shamba kumshauri mkulima namna bora na yenye tija ya uzalishaji wa mazao umshuri mbegu bora umshauri utalaamu mzuri wa namna ya kukuzia mbolea kwenye mazao yake ili hatimaye aweza kuvuna mazao mengi kwenye shamba tofauti na mazoea ya nyuma ya kulima eneo kubwa mavuno kuwa kidogo na haikuwa bahati mbaya kwa sababu nyie maafisa kilimo hamuwafikiagi wa kulima kwa sababu ya ukosefu wa vitendea kazi sasa leo Mhe Rais kaleta vitendea kazi nendeni mkafanye kazi” Katibu tawala Toba akiwasisitiza maafisa hao.

Naye Afisa kilimo Mkoa Kagera Louis Baraka amebainisha kuwa Serikali kupitia wizara ya kilimo imekuwa katika jitihada mblimbali za kuongeza tija katika uzalishaji wa mzao mbalimbali ambapo amefafanua kumba kumekuwepo na changamoto kadhaa zanazoyakabili mazao ya kilimo kwa Mkoa Kagera katika uzalishaji ambapo ametolea mfano wa zao la ndizi kuwa inategemewa mkulima kuvuna mkungu wa ndizi kuanzia kilo 25 hadi 30 ila kwa sasa walio wengi wanajikuta wakivuna mkungu wa kilo 5 hadi kilo 10 hivyo hivyo hata kwenye mazao ya mahindi maharagwe na mengine bado uzalishaji siyo mzuri hivyo ameishukuru Serikali kwakuweza kutoa pikipiki hizo zitakazo kuwa mkombozi na msaada mkubwa kwa maafisa ughani katika kuwafikia kwa wakati wa kulima na kuwapa huduma mbalimbali za ughani kama yalivyo makusudi ya Serikali.
Kwingineko maafisa kilimo ngazi ya wilaya mameishukuru Serikali chini ya wizara ya kilimo kwakuona na kuwiwa kuwapatia pikipiki hizo ambazo zilikuwa ni mahitaji yao makubwa make watalaamu wengi wamekuwa wakishindwa kuwafikia kwa wakati wa kulima kwa sababu ya kutokuwa na vifaa vya usafiri kupitia vyombo hivyo wameahidi kwenda kufanya kazi kwa nguvu zao zote katika kuwafikia wakulima kwenye mashamba yao na maeneo mengine.
Baadhi ya maafisa hao kutoka wilaya za Karagwe, Misenyi na Ngara kwa pamoja wameendelea kutoa shukrani kwa Serikali “Mhe Mkuu wa Mkoa tunakuomba utufikishie salamu zetu kwa Mhe Rais Samia sisi kama watalaamu wa kilimo tulikuwa tanadhani tumesahaulika sahaulika lakini sasa kupitia vitendea kazi hivi tulivyovipokea tunaamini na vingine vilivyoahidiwa vitafika tuu tutaweza kufanya kazi nzuri mno na yenye tija” wamesema wakulima hao.










