Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameondoka Jijini Arusha kupitia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA), kurejea Dar Es salaam. Rais Samia Amekuwa Arusha kushiriki kwenye ufunguzi wa Kikaokazi cha Wenyeviti wa bodi na watendaji wakuu wa Taasisi za umma, Kikao kinachofanyika kwa siku tatu kwenye Kituo cha kimataifa cha mikutano cha AICC. Kwenye uwanja wa ndege wa KIA, Rais Samia ameagwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda na Mhe. Nurdin Babu, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
