Home Kimataifa RAIS DKT. MWINYI: ZANZIBAR KUIMARISHA USHIRIKIANO NA KOREA KUSINI KATIKA UTALII, UCHUMI...

RAIS DKT. MWINYI: ZANZIBAR KUIMARISHA USHIRIKIANO NA KOREA KUSINI KATIKA UTALII, UCHUMI WA BULUU NA TEKNOLOJIA

Celebrating 25 Years of NHIF

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar inalenga kuimarisha ushirikiano na Korea Kusini katika utalii, uchumi wa buluu, nishati mbadala, viwanda, teknolojia na elimu.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 27 Oktoba 2026, jijini Yeosu, alipokutana na Meya wa Jiji la Yeosu, Mhe. Seo Young-hak, na kujadili fursa za ushirikiano na uwekezaji.

Katika ziara hiyo, ametembelea kampuni za POSCO na K-Food, pamoja na Maonesho ya Dunia ya Visiwa 2026, kujifunza teknolojia za uzalishaji viwandani na uchakataji wa mwani kwa lengo la kuongeza thamani ya bidhaa na kukuza uchumi wa Zanzibar.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!