Home Kitaifa RAIS DKT. MWINYI ATEMBELEA MAKUMBUSHO YA HISTORIA YA SOKA NA VIVUTIO VYA...

RAIS DKT. MWINYI ATEMBELEA MAKUMBUSHO YA HISTORIA YA SOKA NA VIVUTIO VYA MADRID, UHISPANIA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametembelea Makumbusho ya Historia ya Magwiji wa Soka (LEGENDS: The Home of Football), pamoja na vivutio mbalimbali vya utalii katika Jiji la Madrid, nchini Uhispania, akiendelea na ziara yake nchini humo.

Rais Dkt. Mwinyi akiambatana na Balozi wa Tanzania Ufaransa anayewakilisha pia Hispania,Mhe.Saidi Yakubu ametembelea makumbusho hayo leo, tarehe 11 Oktoba 2026, na kujionea kumbukumbu mbalimbali za historia ya soka duniani, zikiwemo jezi na vifaa vya magwiji wa mchezo huo.

Ziara hiyo inaendana na juhudi za kuendeleza sekta ya michezo kupitia ujenzi wa miundombinu ya kisasa na kuimarisha fursa za vijana kushiriki na kuendeleza vipaji vyao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!