Na Magrethy Katengu
MAMLAKA ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) umesema katika tafiti zao hadi sasa wamegundua futi za ujazo Trilioni 57.54 za gesi na katika visima 44 kati visima 96 na 52 havikukutwa na kitu.
Akizungumza Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu Mamlaka Udhibiti Mkondo wa juu Mafuta na Gesi asilia PURA Mhandisi Charles Sangweni katika Maonyesho ya sabasaba kwenye banda lao amesema kumekuwa na miradi mbalimbali inayotekelezwa hapa nchini na hivi karibuni katika tafiti zao wamegundua katika bahari Maradi wa Madini gesi kuwa katika hali ya kimiminika unaotarajiwa kutekelezwa hivi karibuni. .
“Mkondo wa juu katika mnyororo wa uongezaji wa thamani katika Mafuta na gesi asilia vyote vinachimbwa ardhini na katika uchimbaji huo unaweza kuishia kupata Mafuta yalio mazito au ghafi au ukapata gesi asilia au maji na wakati mwingine kukosa vyote “ amesema Mhandisi
Hata hivyo Mhandisi Charles amesema unapochimba mafuta unayapata yakiwa katika hali ya tope hivyo tope hilo linachakatwa na kubadika linapoingizwa kwenye mtambo ambao ni Mnara ulielekezwa kufuata joto la jua hivyo kusaidia kujichakata na gesi kupanda juu ambapo gesi hutoa mazao ikiwemo dizeli, mafuta ya taa, petroli na lile tope lililobaki linakuwa lami
Mhandisi Charles amesema tafiti hizo zilianza tangu miaka 50 iliyopita na wamegundua gesi, na ni mchanganyiko wa gesi nyingi Methano ambayo ni chanzo cha nishati na visima vilivyochimbwa ni 96 kati ya hivyo 44 ilipatikana gesi huku 52 hakikupatikana kitu gesi iliyogundulika ni maeneo ya Songosongo na Mtwara Kwara, monazibey, na kuunganishwa kupitia visima vilivyochimbwa Songosongo na kuletwa sokoni kupitia miradi miwili na mradi mmoja wa bomba uliojengwa 2000 mpaka 2004 unaojumuisha nchi 16 lina urefu wa kilomita 247.
Mhandisi Sangweni ameelendelea kueleza kwamba gesi tuliyonayo nchini inazalishwa kutoka Songosongo, Monazibey na Kwara na imekuwa ikitumika katika kuzalisha umeme wa viwandani, majumbani na kadhalika pia asilimia 60 ya umeme tunaotumia nchini inatokana na gesi.
“Sisi ndiyo tutakahusika kusimamia na kudhibiti Mradi mkubwa unaokuja wa kuchakata gesi kutoka hali ya Gesi na kwenda katika hali ya kimiminika” amesema Mhandisi.
Hata hivyo amesema wamekuwa na mikataba hiyo 11 na mikataba miwili imeshaingia kwenye uzalishaji ulishaanza tangu 2014 ambapo gesi iligunduliwa
Aidha kuwa katika tafiti zao hadi sasa wamegundua futi za ujazo Trilioni 57.54 za gesi na uzalishaji unaendelea
Amesema kuwa kama PURA ndiyo Mamlaka ambayo inamshauri Waziri wa Nishati katika Uwekezaji wa nisahti ya mafuta na gesi katika Mkondo wa juu na wanatoa ushauri kwa Waziri wa Nishati na kutoa Leseni ya uchimbaji wa gesi kwa wawekezaji.









