Home Kitaifa POLISI DODOMA WATHIBITISHA MAUAJI YA MC PILIPILI, UCHUNGUZI UNAENDELEA

POLISI DODOMA WATHIBITISHA MAUAJI YA MC PILIPILI, UCHUNGUZI UNAENDELEA

Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma limethibitisha mauaji ya Emmanuel Mathias, maarufu kama MC PILIPILI, mkazi wa Swaswa jijini Dodoma, aliyefariki dunia Novemba 16, 2025. Taarifa hiyo imetolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, ACP William Mwamamfupa.

Akizungumza na waandishi wa habari, ACP Mwamamfupa alisema kuwa msaidizi wa marehemu, Hassan Ismail, alipigiwa simu na mtu asiyefahamika na kuombwa akutane naye. Alipofika eneo la tukio, alikutana na watu watatu wasiofahamika wakiwa na MC PILIPILI ndani ya gari dogo jeupe. Watu hao walimkabidhi MC PILIPILI akiwa katika hali mahututi na kisha kuondoka bila kutoa maelezo.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa awali uliofanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wataalamu wa afya, imebainika kuwa MC PILIPILI alifariki dunia kutokana na kushambuliwa. Uchunguzi zaidi unaendelea ili kubaini wahusika wa tukio hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!