Home Kitaifa NISHATI SAFI YA KUPIKIA YAPIGA HODI SIMANJIRO.

NISHATI SAFI YA KUPIKIA YAPIGA HODI SIMANJIRO.

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) leo, Jumatano tarehe 21 Januari, 2026, umeendelea na usambazaji na uuzaji wa mitungi ya gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku wilayani Simanjiro mkoani Manyara.

Uuzaji na usambazaji umefanyika katika kata ya Mirerani, maeneo ya ofisi ya Mamlaka Ndogo ya Mji wa Mirerani.

Akizungumza wakati wa uuzaji wa mitungi hiyo, msimamizi wa mradi kutoka REA, ndugu Abdulrazack Mkomi, amesema:

Usambazaji na uuzaji wa mitungi ya gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia uliozinduliwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mwezi Mei, 2024.

Aidha, amesema mkakati huo wa nishati safi ya kupikia unaotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita una lengo mahususi la kuboresha maisha ya wananchi kwa kuhakikisha ifikapo mwaka 2034 asilimia themanini (80) ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia.

Vilevile, amesema nishati hiyo safi ya kupikia itasaidia katika uimarishaji na utunzaji wa afya za wananchi, kutunza mazingira na kuleta usawa wa kijinsia katika jamii.

Aidha, mradi huo utasambaza na kuuza mitungi ya gesi 3,255, ambapo mtungi mmoja utauzwa kwa bei ya ruzuku ya shilingi 17,500, na mwananchi atatakiwa kuja na Kitambulisho cha Taifa (NIDA).

Halikadhalika, wananchi wa kata ya Mirerani wameipongeza na kuishukuru Serikali pamoja na REA kwa kuwezesha upatikanaji wa mitungi ya gesi, pamoja na usimamizi mzuri wa mradi, na kuahidi kutumia fursa ya upatikanaji wa mitungi ya gesi ya ruzuku kujiletea maendeleo na kuboresha ustawi wa maisha yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!