Home Kitaifa Ndejembi Akagua Ujenzi Wa Soko La Kirumba, Ataka Michango Ya Nssf Iwasilishwe...

Ndejembi Akagua Ujenzi Wa Soko La Kirumba, Ataka Michango Ya Nssf Iwasilishwe Mara Moja

Celebrating 25 Years of NHIF

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuhakikisha Mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa Soko la Kirumba anawasilisha mara moja michango ya wafanyakazi katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Ametoa agizo hilo leo, tarehe 24 Novemba 2026 alipokagua mradi huo wilayani Ilemela, jijini Mwanza.

Ujenzi wa mradi huo, unaojumuisha barabara ya kilomita 2.9 inayoelekea sokoni, umefikia asilimia 76.6. Ndejembi alieleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi ikilinganishwa na miradi mingine ya TACTIC aliyokagua. Aliutaka uongozi wa Mkoa wa Mwanza kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati na fedha zilizotolewa na Serikali zinatumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa.

FAHARI AFYA

Wakati wa ukaguzi huo, wafanyakazi walilalamika kuwa michango yao ya NSSF imekuwa ikikatwa kwenye mishahara yao bila kuwasilishwa kwenye mfuko. Ndejembi mbali na kumwagiza kufuatilia suala hilo na kumpatia pia alisisitiza kuwa kuwasilisha michango hiyo ni wajibu wa mwajiri kwa mujibu wa sheria na kwamba wafanyakazi wanapaswa kupata uthibitisho kuwa NSSF imeipokea.

Akijibu hoja hiyo, mwakilishi wa mkandarasi, China Railway 15 Bureau Corporation, Bw. Faraja Kabuga, alisema kampuni imekuwa ikiwalipa wafanyakazi mishahara na stahiki nyingine kwa wakati, huku michango yao ya NSSF ikiwa bado haijawasilishwa. Alisema mkurugenzi mtendaji wa kampuni ameidhinisha malipo na ameahidi kuwa michango yote inayodaiwa tangu mradi ulipoanza itawasilishwa kabla ya tarehe 30 mwezi huu.

Mradi wa soko la Kirumba, unagharimu TSh bilioni 14.7 na unatarajiwa kukamilika Januari 2027. Soko litakapokamilika litakuwa na maduka 148, migahawa minane na ofisi saba za utawala.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!