Home Kitaifa MTEMVU: SIMAMENI NA KUIELEZEA MIRADI ILIYOTEKELEZWA NA SERIKALI.

MTEMVU: SIMAMENI NA KUIELEZEA MIRADI ILIYOTEKELEZWA NA SERIKALI.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar Es Salaam ABAS MTEMVU amewataka wanachama wa CCM kusimama na kuelezea miradi iliyotekelezwa na serikali katika maeneo yao

Ametoa wito huo wakati akizungumza na jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi wilaya ya ubungo mkoa wa Dar es salaam leo Januari 28, 2023, katika mkutano ulioandaliwa na umoja huo.

Akizungumza na vijana hao, Mtemvu amesema wanatambua vyama vigine vimejiandaa kwa mikutano, Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakitajibu kwa kutukana kitajibu kwa kuelezea yale ambayo serikali ya Dkt SAMIA SULUHU HASSAN imeyafanya.

Aidha Mtevu amewataka kila kijana mwenye uwezo wa wakufanya biashara watengeneze makundi wawezeshwe “tunapenda vijana wote kama hampo maofisini basi muwe na kazi zenu wenyewe za kujiajiri fedha zipo manispaa tengenezeni makundi wataalamu wapo

Hata vivyo awewahasa vijana hao warejeshe mikopo waliyopewa ili iweze kuwasaidia wengine “zile fedha mnazopewa unafanyia wewe ukimaliza unarejesha anapewa mwenzio” amesema

Kwa upande wake Mwenyekiti Wa Umoja Wa Vijana Mkoa wa Dar es Salaam NASRA RAMADHANI amewasihi vijana kudumisha umoja kama ilivyo dhana ya chama cha mapinduzi na kuwaomba viongozi wa chama na jumuiya wa mkoa huo kuendelea kusimamia ilani ya chama cha mapinduzi kwa vitendo ili kupelekea kuleta maendeleo.

Naye Mwenyekiti Wa Umoja Wa Vijana Wilaya ya Ubungo SHEDRACK MAKANGULA awewataka vijana kuendelea kuwa mtari wa mbele kuendelea katika kukitetea chama cha mapinduzi na kuisemea serikali ya awamu ya sita kwa kazi nzuri inayoifanya

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!