Home Kitaifa MIRADI YA BILIONI 56 YATEKELEZWA GEITA DC, BARAZA LA MADIWANI LAJIPONGEZA

MIRADI YA BILIONI 56 YATEKELEZWA GEITA DC, BARAZA LA MADIWANI LAJIPONGEZA

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuongeza mapato ya ndani kutoka vyanzo vyake hadi kufikia zaidi ya shilingi bilioni 10 katika kipindi cha miaka mitano, ongezeko linalokadiriwa kuwa asilimia 120.62.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Karia Rajabu Magaro, wakati wa mkutano maalum wa kuhitimisha Baraza la Madiwani kwa kipindi cha miaka mitano. Magaro amesema mafanikio hayo ni matokeo ya usimamizi thabiti wa rasilimali pamoja na mshikamano wa viongozi na watendaji wa halmashauri hiyo.

Aidha, miradi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 56 imetekelezwa katika kipindi hicho, ikihusisha fedha za ndani pamoja na michango ya wadau wa maendeleo.

“Ni jambo la kujivunia kuona jinsi madiwani walivyoshirikiana kwa dhati kuhakikisha maendeleo yanapatikana. Kila mmoja ana sababu ya kujipongeza kwa kazi kubwa iliyofanyika,” alisema Magaro.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Dkt. Charles Kazungu, amesema hatua kubwa za maendeleo zilizofikiwa ni zao la uongozi bora chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Rais Samia ameendelea kufungua fursa mbalimbali kwa Watanzania, ikiwemo kuhakikisha daraja la Magufuli linafunguliwa rasmi na kuanza kutumika, jambo lililowezesha kurahisisha usafiri na kukuza uchumi wa eneo letu,” alisema Dkt. Kazungu.

Baraza hilo maalum limehitimisha kipindi cha miaka mitano cha utumishi wa madiwani, huku viongozi na wananchi wakipongeza jitihada zilizofanikisha maendeleo katika sekta mbalimbali ndani ya wilaya hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!