
Na Shomari Binda-Musoma
MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amesema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameshawafikia wananchi wa Musoma na kuwawezesha kiuchumi.
Kauli hiyo ameitoa leo disemba 30 aliposhiriki na kuzunhumza kwenye kongamano la jukwaa la uwezeshaji wananchi kiuchumi Wilaya ya Musoma lililofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Mukendo.
Jukwaa hilo ni muendelezo wa matukio ya Mama Samia Musoma Festival ilyoandaliwa na ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Musoma.
Mathayo amesema kupitia sekta ya uvuvi pekee Tais Dkt.Samia kwa manispaa ya Musoma ametoa vizimba na chakula cha samaki ikigharimu zaidi ya bilioni 1.

Amesema licha ya eneo hilo la uvuvi tayari halmashauri ya manispaa ya Musoma imeanza kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake,vijana na wenye ulemavu.
Mbunge buyo amesey hizo zote ni fursa za kuwawezesha wananchi kiuchumi ambazo wanapaswa kuzitumia na kujiinua.
Amesema wananchi wanapaswa kuacha uvivu na kujituma kufanya kazi ili fursa zilizotolewa ziweze kuwainua.

” Nikushukuru sana mkuu wa Wilaya ndugu yangu Chikoka kwa kuandaa jambo hili na kukutana kuweza kukumbushana.
” Mama Samia Musoma ameshatufikia katika kutuwezesha kiuchumi na sasa ni jukumu letu kuendelea kuwahamasisha wananchi kuzitumia”amesema.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amesema lengo la jukwaa hilo ni kukumbushana na kuelezana fursa za uchumi zilizopo.