Na Theophilida Felician Kagera.
Mbunge wa Jimbo la Bukoba mjini na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Stephen Byabato amefanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha waendesha pikipiki maarufu boda boda wanapata mikopo ya pikipiki kwa gharama nafuu na masharti nafuu kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwemo wa Benki.

Byabato amesema hayo kwenye Mkutano wake na waendesha pikipiki katika viwanja vya Kaitaba mjini Bukoba ambapo amesema kuwa amefanya hivyo ili kuwakwamua madereva hao katika kujiongezea kipato kiuchumi pamoja na kuwasaidia kuziepuka changamoto wanazokumbana nazo kwenye mikataba umiza ya pikipiki wanazofanya nazo kazi za mikataba ya watu binafsi.
Ameeleza kwamba katika jitihada hizo amekubaliana na Benki ya NMB kuwakopesha pikipiki madereva hao kwa atakaye kuwa tayari baada ya kuona gharama zao na masharti yao ni na fuu hivyo kwa atakaye changamkia fursa hiyo atanufiaka zaidi kutokana na mikopo hiyo yenye kuhitaji kianzio cha 20% ya pikipiki inayohitajika.

Amesema kuwa yeye kama Mbunge ameanza kwa kulipa 10% kwa pikipiki 15 kwa vijana watakaojiwahi nakuongezea 10% ili ikamilike 20% na weweze kupewa pikipiki kutoka katika Benki hiyo ya NMB ndani ya muda wawiki moja.
Hata hivyo ameongeza kuwa ameileta mbinu hiyo ili iwasaidie kumiliki pikipiki zao wenyewe na kuondokana na pikipiki za watu ambao wamekuwa wakiwanyanyasa kupitia mikataba umiza pili itawasaidia kuepuka na masuala ya uhalifu huku akiwasihi kuziendesha kwa kutii sheria za usalama barabarani.
Kwa upande wake afisa mikopo mikubwa na midogo pamoja na kilimo kutoka NMBJoanita Ijumba amesema kwamba mikopo hiyo ni nafuu sana ambapo kwa atakaye kuwa anahitaji sharti la kwanza awe kwenye kikundi kilicho sajiliwa.
Mikopo ya pikipiki hizo amesema ni pamoja na pikipiki za Sh Milioni mbili na laki tisa pamoja na ya pikipiki za Sh Milioni Mbilili na laki Saba.
Joanita amefafanua kuwa dhamana ya pikipiki ya Milioni ya mbili na laki tisa ni Sh laki tano na Elfu themanini tuu na kwa pikipiki ya Milioni mbili na laki Saba dhamana yakeni ni Sh laki tano na Elfu alobaini tuu.
Ameendelea kueleza kuwa marejesho yake yatakuwa ni Sh Elfu alobaini na tano kwa wiki badala ya Elfu Sabini wanayoilipa kwa watu binafsi na baada ya mwaka mmoja pikipiki itabakia kumilikiwa moja kwa moja na mkopeshwaji hivyo amewasi sana waendesha pikipiki wa Bukoba kujiunga kwenye vikundi ili iwe njia rahisi ya kuwawezesha kunufaika na pikipiki hizo kwani zipo kwa ajili yao.
Naye Mkuu wa wawilaya Bukoba akiwa Mgeni rasimi katika Mkutano huo Mhe Erasto Sima amewahimiza madereva hao kufanya kazi zao kwa kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepukana na misuguano na Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabani sambamba na kutokushiriki vitendo viovu vya kiuhalifu kwani atakayebaini akihusika na matukio hayo atakumbana na mkono wa sheria.
Nao madereva hao wamemshukuru Mbunge Byabato kwa kuja na mkakati huo mzuri kwao hivyo wamemuomba kuendelea kuwaunga mkono kwa namna yoyote ile ili malengo hayo yaweze kutimia kwani wanatamani kila mwendesha pikipiki wa Jimbo hilo aweze kunufaika na mikopo ya pikipiki hizo licha ya uwezo wakipato kuwa mgumu.








