Na Magrethy Katengu
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekuja na suhisho la risiti halali kwa kampeni inayojulikana kwa jina la “Tuwajibike” itakayosaidia kuwakumbusha na kuwahamasisha wauzaji bidhaa na wananunuzi kutoa na kudai risiti halali za EFD hususani biashara za usafirishaji wa vipeto na vifurushi .
Akizungumza na Waandishinwa Habari wakati akitambulisha kampeni hiyo Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma na Elimu kwa mlipakodi Richard kayombo amesema baadhi ya Wafanyabiashara wamekuwa vidhaa zao zimekuwa sugu kwabutoaji risiti ambazo ni usafirishaji wa vipeto na vifurushi na sehemu za starehe zimekuwa hazitoi risiti hivyo kupitia kampeni hiyo watu wao watakuwepo kwenye maeneo ya biashara hivyo wasiseme wameshtukizwa maana elimu hiyo ilishatolewa na sio sheria mpya.
Hata hivyo amesema kampeni ya Tuwajibike ni kampeni yenye malengo makuu matatu ikiwemo kuwakumbusha na kuwahamasisha wauzaji wa bidhaa na watoa huduma nchi nzima kuwajibika kwa kutoa risiti halali ya EFD kila wauzapo bidhaa au kutoa huduma.
“Kampeni hii tumelenga kuwakumbusha na kuwahamasisha wanunuzi wa bidhaa na huduma kote nchini kuwajibika kudai risiti halali za EFD pamoja na kuzikagua ili kujiridhisha kuwa inakidhi vigezo vyote muhimu na pia itahusisha kufuatilia utoaji wa risiti halali za EFD nchi nzima pamoja na kuchukua hatua kwa wauzaji wasiofuata sheria katika utoaji wa risiti”amesema Kayombo.
Sanjari na hayo amesema baadhi ya vitu vinavyoashiria udanganyifu ni kudai mashine za EFD mbovu bila udhibitisho na kutumia risiti moja kusindikiza mzigo kutwa nzima hususani vifaa vya ujenzi, risiti ni halali ila bei ni tofauti na mteja aliyolipa pamoja na wanaotafuta mashine za EFD kwa lengo la kufyatua risiti na kuwapa watu risiti hewa kwa kudai fedha na hakuna biashara wanayofanya.
”Risiti halali ya EFD inatakiwa kukidhi vigezo vikuu vinne (4) ambavyo ni jina la biashara,tarehe halisiya mauzo,kiasi halisi cha pesa kilichonunuliwa bidhaa au TIN ya mnunuzi au vyote kwa pamoja” Alisema kayombo.
Sambambana hayo amesisitiza kuwa adhabu itachukuliwa kwa yeyote atakaebainika kufanya udanganyifu ambapo kwa mfanyabiasha atakayebainika kutokutoa risiti halali ya EFD au kufanya udanganyifu atatozwa faini ya Shilingi 3,000,000/= mpaka Shilingi 4,500,000/= au kifungo kisichozidi miaka mitatu au vyote kwa pamoja.
Aidha kwa mnunuzi atajayebainika kufanya manunuzi bila kudai risiti halali ya EFD atatozwa faini ya kuanzi Shilingi elfu 30 hadi milioni moja na nusu au kifungo cha miaka mitatu au vyote kwa pamoja.








