Na. Khadija Seif
MAPROMOTA waombwa kutazama vipaji vya Mabondia wachanga mtaani ili viweze kupewa nafasi ya kuonekana ili kubadilisha mchezo wa Masumbwi na kuwa na Mabondia wengi wenye mafanikio na majina nje na ndani ya nchi.
Promota huyo amebainisha mabondia hao ni Oscar Richard dhidi ya Adam Mbega, Emmanuel Mwakyembe atapigana na Francis Miyeyusho, Mbaraka Mtange atazichapa na Hamza Mchanjo, Alex Kachelewa dhidi ya Adam Mrisho, Mwinyi Mzengela kumenyana na Ajemi Amani.
Wengine Abdul Kubila dhidi ya Msabaha Salum, Omary Baraka kupigana na Muksini Kizota, Ahmady Pelembela dhidi ya Iddy Pazzy wakati Frola Machela atacheza na Halima Bandola.
Bondia Selemani Kidunda amesema kutokana na maandalizi mazuri anayofanya, watanzania wategemee ushindi kutoka kwake. Pambano linalokuja ataonyesha vitu vya utofauti ambapo watanzania na wadau wa ngumi hawajawahi kuona.
“Nimejipanga na naendelea na mazoezi, bondia ninayeenda kucheza naye ni mzuri, lakini atapigwa na mkanda utabaki nyumbani.”
Kidunda mwenye umri wa miaka 39, anapanda ulingoni akiwa na kumbukumbu ya kushinda pambano ya Kidemkrasi ya Congo (DRC), pambano hilo lilofanyika Julai mwaka jana, Songea mkoani Ruvuma.








