Home Kitaifa KIBAHA KUWA MANISPAA: KOKA ATAJA CHANGAMOTO YA MAJI KATA YA PANGANI

KIBAHA KUWA MANISPAA: KOKA ATAJA CHANGAMOTO YA MAJI KATA YA PANGANI

WAZIRI wa Tamisemi Mohamed Mchengerwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanja Samia Suluhu Hassan ameridhia kupandiaha hadhi Halmashauri ya Mji wa Kibaha kuwa Manispaa.

Mchengerwa ameyasema hayo Januari 27 aliposhiriki hafla ya kuunga mkono maazimio ya Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kumpitisha Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea pekee wa Urais pamoja na mgombea Mwenza Balozi Emmanuel Nchimbi huku upande wa Zanzibar Hussein Mwinyi akiteuliwa kuwa mgombea Urais Zanzibar.

Akiwa katika hafla hiyo ilivyofanyika Mailimoja Mjini Kibaha Waziri Mchengerwa ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa alitokea Mkoa wa Pwani amesema Rais ameridhia ombi hilo na kwamba michakato mingine itaendelea kukamilisha miradi.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Ramadhani Mlao alisema chama hicho kwa mkoa huo kinaungana na maazimio ya Mkutano Mkuu kwa wagombea waliopitishwa kugombea nafasi ya Rais Bara na Zanzibar katika uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Sylvestry Koka amemshukuru Rais kwa kuridhia kupandisha hadhi Halmashauri hiyo na kuwa Manispaa baada ya maombi ya muda mrefu.

Koka amesema hayo yote yametokana na Maendeleo yaliyofanyika na kwamba wanaendelea kujenga mji huo kama ambavyo umekwisha kupangwa Ili uendelee kuwa wa kisasa.

Amesema yaliyofanyika tangu aingie madarakani 2010 ni mengi katika mji wa Kibaha jambo ambalo linastahili Halmashauri hiyo kuwa Manispaa na kwamba kwasasa barabara za lami zimeongezeka kwa kila kata ukilinganisha na miaka ya nyuma.

Koka amesema Changamoto pekee iliyobaki kwasasa ni maji katika kata ya Pangani ambayo inaendelea kushughulikiwa na hivi karibuni itatatuliwa.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!