Home Biashara KAMILISHENI JENGO LA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA KWA WAKATI

KAMILISHENI JENGO LA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA KWA WAKATI

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt Selemani Jafo amemuagiza Mkandarasi Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuongeza kasi ya ukamilishaji wa jengo la wizara hiyo kwa wakati.

Dkt Jafo aliyasema hayo wakati alipotembelea Jengo la Wizara hiyo kugagua ujenzi uaoendelea mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara hiyo Julai 08, 2024 Mtumba Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo hilo, Dkt Jafo alisema mkandarasi anapaswa kuongeza kasi ya kukamilisha ujenzi wa jengo hilo ifikapo Septemba 30 mwaka huu ili wafanyakazi wote  wa Wizara hiyo wahamie kwenye jengo jipya la wizara.

Nimefanya ukaguzi wa jengo hili la wizara nimeona kazi inaenda vizuri na ikifika Septemba kazi zote zimekamilika, hivyo Mkandarasi ongeza kasi ya kukamilisha ili ikifika Septemba 30 mwaka watumishi tuweze kuingia.”

Mwaka 2021, Serikali ilianza ujenzi wa awamu ya pili wa majengo ya ofisi za wizara na taasisi ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa adhima ya Serikali ya kuhamia Dodoma ulioanza mwaka 2016.

Kwa takwimu zilizopo, tayari watumishi 25,039 kutoka Serikali kuu, bunge, mahakama, vyombo vya Ulinzi na Usalama, pamoja na taasisi 65 wameshahamia  na wanaendelea kutekeleza majukumu yao wakiwa Dodoma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!