Na Theophilida Felician Kagera.
Jeshi la polisi Mkoa Kagera limesema kuwa limewaua watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi na kufanikiwa kukamata silaha moja ya Bunduki aina ya( AK47) ikiwa na magazine yenye risasi 25 .
Akizungumzia juu ya tukio hilo kwa vyombo vya habari ofisini kwake Manispaa ya Bukoba kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Kagera Williamu Mwampaghale ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea mnamo terehe 21 January mwaka huu huko eneo la Kumnazi wilaya Ngara.
Amefafanua kwamba tarehe 21 Jeshi la polisi lilipata taarifa za kuwepo kwa kikundi cha watu wanaopanga kufanya matukio ya uhalifu wakutumia silaha ambapo jeshi hilo lilitega mitego katika maeneo ya barabara zote za kuingia mji wa Ngara hivyo majira ya saa 3:35 usiku katika barabara ya kutoka hapo Kumnazi kuelekea Rulenge kulijitokeza watu watatu waliokuwa wamepanda pikipiki ambapo Askari waliokuwa katika doria waliwasimamisha watu hao na wakakaidi kusimama badala yake waligeuza pikipiki nyuma walikokuwa wakitokea ili wakimbie.
“Polisi walifyatua risasi hewani wakizidi kusisitiza wasimame lakini bado walikaidi ndipo Polisi waliamua kupiga risasi za hewani japo ziweze kunasa taili za pikipiki pengine isiendelee na safari kwa bahati mbaya risasi hizo ziliwapata watu wawili mmoja sehemu ya paja la mguu wa kushoto na wapili sehemu ya kiuno hali iliyowapekea kudondoka chini kutoka kwenye pikipiki ile na mtu watatu alifanikiwa kukimbia na kutokomea na pikipiki ambayo hatukuweza kuitambua kwani alizima taa zote” amesema kamanda Mwampaghale.
Eneo la tukio Baada ya kufanya upekuzi kwenye makoti waliyokuwa wameyavaa watu hao walikutwa na silaha moja ya bunduki aina ya (AK47) ikiwa na magazine moja yenye risasi (25) sambamba na mambomu (2) ya kurushwa kwa mkono.

Ameongeza kuwa watu hao ambao hawajatambulika majina yao wenye umri kati ya mika 25 hadi 30 walifariki wakiwa njiani kupelekwa katika Hosptali ya Nyamiaga wilaya Ngara na mili yao bado imehifadhiwa katika hosptali hiyo kwa uchunguzi.
Kamanda Mwampaghale ametoa onyo kali akiwataka watu wote wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu hususani uhalifu wakutumia silaha waache mara moja kwani operesheni na misako mikali itaedelea ili kuhakikisha wanakamatwa na kufikishwa mahakamani huku akitoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano wakutoa taarifa sahihi za watu wa namna hiyo na waweze kudhibitiwa mapema kabla ya kusababisha madhara.

            







