Home Kitaifa “IPO MIGOGORO ILIYOTUSHINDA TUMEKUJA KUKATA RUFAA” RC MAKONDA

“IPO MIGOGORO ILIYOTUSHINDA TUMEKUJA KUKATA RUFAA” RC MAKONDA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Paul Christian Makonda ametoa Wito kwa Wananchi wa Mkoa wa Arusha wenye migogoro mbalimbali ikiwemo ya Ardhi,Mirathi, Ndoa, Matunzo na Malezi ya Watoto, Ukatili na Unyanyasaji wa Kijinsia, Migogoro ya Madai na Uhitaji wa Elimu ya Msaada wa Kisheria kuitumia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Legal Aid kuwasilisha kero zao.

Makonda amesema hayo wakati akizungumza na timu ya Wataalam waliofika katika Mkoa wa Arusha na ambao wanaanza kutoa Huduma za Msaada wa Kisheria kuanzia tarehe 1 Machi, 2025 kuelekea katika Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Mwanamke ambayo Kitaifa yatafanyikia jijini Arusha.

Mkuu wa Mkoa Mhe. Makonda amesisitiza Timu hiyo ya Mawakili kuhakikisha kuwa inawasikiliza Wananchi kwa Utulivu na kufuatilia changamoto zao kwa kina ila kupata ufumbuzi wa Kudumu katika migogoro inayowakabili na kupunguza msongamano wa Wananchi wanaofika Ofisi wakiwa na migogoro ya aina mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!