Home Kitaifa MIJADALA MIKUBWA YAKUBORESHA UFUNDISHAJI NA UJIFUNZAJI WA ELIMU KUFANYIKA MUSOMA VIJIJINI

MIJADALA MIKUBWA YAKUBORESHA UFUNDISHAJI NA UJIFUNZAJI WA ELIMU KUFANYIKA MUSOMA VIJIJINI

Na Shomari Binda-Musoma

KONGOMANO kubwa la mijadala ya uboreshaji na ufundishaji kujenga uelewa kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari litafanyika kwa siku 3 jimbo la Musoma vijijini.

Wataalamu wa elimu watakaoongoza kongamano hilo litakalofanyika machi 25 hadi 27 jimboni humo ni Dr. Zablon Kengera kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
Dr. George Kaangwa, UDSM na nduguJeff Makongo mtaalam wa ubunifu (Ubunifu Associates)

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo februari 28/2025 mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof Dr.Sospeter Muhongo atagharamikia matukio hayo kwa siku hizo 3.

Taarifa hiyo imedai mjadala wa kwanza utafanyika machi 25 2025 Busambara Sekondari
washiriki waÄ·iwa maafisa elimu Kata 21 wataalam na wadau wengine wa elimu

Mjadala wa pili utafanyika machi 26 2025 Busambara shule ya msingi kuanzia saa 3 asubuhi hadi Saa 6 washiriki wakiwa walimu wakuu 120 na wataalamu 3 na baadae saa 8 mchana hadi Saa 11 jioni
(Secondary Education)
washiriki wakiwa wakuu wa sekondari 32 na wataalam 3

Siku ya mwisho machi 27/2025 mjadala utafanyika makao makuu ya Halmashauri yaliyopo Suguti Kwikonero
Washiriki wakiongozwa na mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka,DED, DEOs,madiwani mbunge wa Jimbo Profesa Sospeter Muhongo na wataalamu 3 na washiriki kutoka kwenye shule za serikali na binafsi wakikaribishwa.

Mijadala ya miaka ya nyuma
mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini amekuwa akifadhili mijadala yenye malengo kama haya na in machi 2025 ambayo ni 2019 mjadala wa mkoa wa Mara 2021 mjadala wa wakuu wa sekondari za Musoma.

Aidha taarifa hiyo imewaomba wadau wa elimu kuendelea kuchangia kuboresha sekta hiyo kwenye jimbo la Musoma vijijini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!