Home Kitaifa GSM GROUP YAENDELEZA KONGANI YA VIWANDA

GSM GROUP YAENDELEZA KONGANI YA VIWANDA

Mradi wa Kilimanjaro Industrial Park umeendelea kuonyesha mchango mkubwa katika kukuza sekta ya viwanda na utoaji wa ajira, ambapo ukikamilika unatarajiwa kutoa ajira hadi 30,000 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, huku kwa sasa ukitoa ajira takribani 5,000.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, alipofanya ziara katika kongani hiyo inayomilikiwa na makampuni ya GSM tarehe 22 Januari 2026 jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji na kusikiliza changamoto zinazowakabili wawekezaji wa ndani.

Katika ziara hiyo, Waziri Kapinga amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi yaliyochochea ukuaji wa uwekezaji wa ndani na nje ya nchi, huku serikali ikiendelea kushirikiana na Wizara ya Nishati na TANESCO kuboresha upatikanaji wa umeme viwandani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa GSM Group, Aisha Mohamed, amesema mradi wa Kilimanjaro Industrial Park una ukubwa wa karibu eka 300 na utakuwa na viwanda zaidi ya 20, huku mfanyakazi wa kiwanda hicho, Eliya Nada Dambay, akiishukuru serikali kwa kuendeleza viwanda vilivyowawezesha vijana kupata ajira, mafunzo na vipato.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!