Home Michezo FRIENDS OF TULIA TRUST  WASHINDWA KUTIKISA NYAVU ZA ESPANYOL 

FRIENDS OF TULIA TRUST  WASHINDWA KUTIKISA NYAVU ZA ESPANYOL 

Na. Munira Abdallah, Mzawablog

KATIKA  Muendelezo wa Ligi ya Sodo 4 Climte timu ya Friends of Tulia trust wayaaga Mashindano rasmi kwa upande wa Wanawake na  Wanaume. 

Akizungumza Afisa Habari wa Kampuni ya Betika Juvenalius Rugambwa amesema Ligi imefanyika katika Fukwe za Coco Beach ambapo Mtanange huo ulishirikisha timu takribani Timu 08.

Hata hivyo Rugambwa ameeleza kuwa Mchezo huo  kati ya Friends of Tulia trust dhidi ya Espanyol zilihusisha upande wa Timu ya Wanawake na Wanaume huku Friends of Tulia trust wakiambulia patupu na kuyaaga mashindano hayo.

Sodo upande wa wanawake Friends of tulia 1-2 Espanyol, katika sodo wanaume friends of Tulia Trust 0-2 Espanyol. Hivyo Friends of tulia trust tayari wameaga mashindano rasmi “.

Pia amesema Mchezo unaofata ni timu ya Mkuu wa Mkoa (RC Fc ) dhidi ya Bodaboda fc kutoka Msasani anbapo Mchezo huo utafanyika Fukwe za Coco Beach machi 04,2023.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!