Home Kitaifa EWURA CCC YAWASISITIZA WATUMIAJI WA VYOMBO VYA MOTO KUTIMIZA WAJIBU WA KUDAI...

EWURA CCC YAWASISITIZA WATUMIAJI WA VYOMBO VYA MOTO KUTIMIZA WAJIBU WA KUDAI RISITI

Na Theophilida Felician Kagera.

Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za nishati na maji Mkoa Kagera EWURA CCC limewakumbusha na kuwahimiza watumiaji wa vyombo vya moto Mkoani humo kuhakikisha wanadai risiti kwenye vituo wanavyonunulia mafuta ya vyombo vya moto.

Akizungumza na Blog hii katika makao makuu ya ofisi za baraza hilo Manispaa ya Bukoba Afisa huduma kwa wateja msaidizi na utawala Anadorice Komba amesema kuwa wakati mwingine hujitokeza changamoto mbalimbali kwa watumiaji wa vyombo vya moto wanapokuwa wamenunua mafuta kwenye vituo husika hivyo wengi wao hushindwa kutatuliwa matatizo yao wafikapo kulalamika katika ofisi hizo kutokana na kutokuwa na risiti zenye vielelezo vya ushahidi wa manunuzi ya kile wanachokilalamikia kutoka kwa watoa huduma.

“Tunasema kuchukuwa risiti pindi unapopata huduma ya mafuta yawe ya petroli ama ya taa ni muhimu sana ukifanya hivyo kwa usahihi itakusaidia pale ambapo unalalamika baada ya kupata madhara pengine kutokana na mafuta uliyoyanunua kwenye kituo husika kwa mfano umewekewa mafuta ya taa machafu au umenunua mafuta bei ambayo siyoelekezi kwa hiyo usipokuwa na risiti haki yako itapotea kwa sababu unapokuja kwetu kulalamika kwamba labda kituo (A) kimeniuzia mafuta machafu na yamesababisha madhara kwenye chombo changu cha kwanza tutakuomba risiti sasa kama huna rusiti matokeo yake hatutaweza kwenda hatua nyingine itakuwa imeishia pale utapoteza haki yako maana risiti hiyo itakuwa na vielelezo vyote ikionyesha kituo husika ni kwa muda gani umefanya manunuzi ya ghalama kiasi gani na mengine”amesema Anadorice Komba.

Ameeleza kuwa ofisi hiyo hupokea malalamiko mara kadhaa japo siyo kwa wingi hivyo yenye kuwa na risiti huyashughulikia kwakuwafikia watoa huduma wanaolalamikiwa ili kubaini chanzo cha lalamiko lenyewe hatimaye kufanyiwa utatuzi.

Afisa huyo amefafanua kuwa watumiaji wa vyombo vya moto hususani kwa upande wa pikipiki wengi wao hawadai risiti kabisa kwa madai kuwa hununua mafuta kidogo kidogo kila siku kwa hiyo watajikuta wakijaza risiti hizo kwa wingi na hali hiyo huwapelekea kupuuza zoezi hilo kwa maana kwamba zikiwa nyingi na utunzaji wake inakuwa kazi ngumu kwao jambo ambalo siyo zuri na salama kwa vyombo vyao.

Ameongeza kuwa baraza hilo limekuwa likifanya juhudi za kila aina katika kuwafikia wananchi wote na kuwapa elimu kama yalivyo majukumu yao ya kila siku huku akiwasihi wananchi wakiwemo waendesha vyombo vya moto kushiriki vyema pindi wanapowafikia maeneo tofauti tofauti kwa ajili ya utoaji elimu ya utumiaji wa huma za nishati na maji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!