Mkuu wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro Mheshimiwa Shaka Hamdu Shaka akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani cha kujadili na kupitisha bajeti kwa mwaka 2023/2024 ya Halmashauri ya Kilosa Jana Alhamisi Februari 16, 2023 kilichofanyika katika Ukumbi wa Madaraka ameeleza mikakati na mipango ya kukabiliana na migogoro ya ardhi kwenye wilaya hiyo.

“Tumejipanga na tunakuja na mkakati kabambe kumaliza Migogoro ya wakulima na wafugaji, nataka tuandike pamoja historia ya kumaliza kabisa changamoto ya migogoro hii Kilosa. Namimi nikiwa Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hii nitaanza na watendaji ndani ya Serikali ambao ni sehemu ya ustawi au wanufaika wa migogoro hiyo, hivyo niwahahakishie kama kuna mtu yeyote miongoni mwetu, anafaidika na migogoro hii ama anahusika kwa namna moja ama nyingine kuistawisha atakutana na mkono mkali wa sheria kwenye hili hatutangaliana usoni”
Kauli ya DC Shaka Hamdu Shaka wakati akiweka msisitizo asubuhi Alkhamis 16 Februari 2023 alipokuwa akiongea na Madiwani katika kikao cha Baraza la Halmashauri ya Wilaya Kilosa ambapo wakati wa jioni alipata fursa kufika eneo la Magomeni ambako wananchi walifikisha malalamiko yao ofisini kwake jana.










